Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Pacers ilivyofufuka mchezo wa kwanza

Muktasari:

  • Vita kubwa kwenye fainali ya NBA, ilikuwa kati ya mashambulizi ya Pacers dhidi ya ulinzi wa Oklahoma City Thunder. 

OKLAHOMA, MAREKANI: INDIANA Pacers imefanya yake, lakini safari hii imefanya dhidi ya ngome imara zaidi ya ulinzi katika Ligi ya Kikapu Marekani.

Vita kubwa kwenye fainali ya NBA, ilikuwa kati ya mashambulizi ya Pacers dhidi ya ulinzi wa Oklahoma City Thunder. 

Indiana iliupindua mchezo kwa kishindo baada ya kuwa nyuma kwa alama 15 mapema katika robo ya mwisho na hatimaye kuibuka na ushindi wa kushtukiza wa pointi 111-110 dhidi ya Thunder ikiwa ni mara ya pili kwa Oklahoma kupoteza dhidi ya timu ya ukanda wa Mashariki msimu huu.

Katika nusu ya kwanza, Indiana ilifunga pointi 45 katika mashambulizi 54, huku ikipoteza mipira mara 19 kikiwa ni kiwango cha juu.

Lakini katika nusu ya pili iliibuka upya, ikifunga pointi 66 katika mashambulizi 48 na kupoteza mipira mara tano.

Dakika 10 kabla ya mchezo kumalizika ikiwa nyuma kwa alama 15, Pacers ilifunga pointi 32 katika mashambulizi  19 ya mwisho, safu iliyohitimishwa na mpira wa ushindi uliopigwa na Tyrese Haliburton kwa sekunde 0.3 kabla ya filimbi ya mwisho.

Huu ni uchambuzi wa kiufundi, takwimu na mikakati iliyoibadilisha Indiana Pacers kutoka kuyumba hadi ushindi mkubwa:


1.  Mtego wa Thunder 

Thunder ni timu inayoongoza kwa kulazimisha makosa ya kupoteza mipira wastani wa makosa 18.1 kwa kila mashambulizi 100, kiwango kikubwa zaidi katika misimu 10 iliyopita ya mtoano. Zaidi ya nusu ya makosa hayo ni “live ball turnovers” yaani makosa yanayowawezesha kupata mpira na kuanzisha mashambulizi ya haraka.

Katika nusu ya kwanza ya mchezo wa kwanza, Thunder ilirekodi makosa 12 ya kuiba mpira rekodi ya nusu moja ya mchezo wa fainali tangu takwimu za kuiba mpira zianze kurekodiwa 1973.

Lakini Pacers ilipoweza kuvunja mtego huo wa Thunder ilipata nafasi nzuri kwenye upande dhaifu wa uwanja. Thunder iliwahi kuruhusu wastani wa mitupo 4.4 kutoka kona moja kwa moja katika msimu wa kawaida, kiwango cha juu zaidi ligi nzima.

Katika mchezo huo, Pacers ilitupia 10 kati ya 16 kutoka kona ikiweka rekodi ya 7 kati ya 9 katika nusu ya pili. Sasa inatupia kwa asilimia 48.5 kwenye kona katika mtoano.

Moja ya mifano bora ni pale Haliburton alipotumia ujanja dhidi ya Turner, akasita kutupa mpira alipobana na badala yake akampasia Pascal Siakam aliyepenyeza kwa Aaron Nesmith aliyekuwa huru kona ya mbali na akatupia bila presha.


2. Kucheza kwa kubadilisha vipimo

Katika mashambulizi tisa ya kwanza, Pacers ilipata pointi tano, lakini ilifanikiwa kufunga mara mbili kutokana na ‘mismatch’ ya urefu. Siakam alipata nafasi ya kumshusha Cason Wallace (mchezaji wa futi 6 na inchi 3) na kumshinda kwa urefu.

Lakini mchango mkubwa zaidi wa Siakam ulikuja katika dakika za mwisho alipokuwa akiwazidi nguvu wachezaji wa Thunder kwenye mipira ya kurudia.

Kwa mfano dakika 3:24 kabla ya mwisho, Thunder ilikuwa na kikosi kifupi chenye mchezaji mrefu zaidi Shai Gilgeous-Alexander (futi 6 na inchi 6). Siakam alitumia fursa hiyo kupata mpira wa kurudia juu ya MVP huyo, na baada ya kufanyiwa faulo na Wallace alipata pointi moja muhimu.

Na chini ya dakika moja kabla ya mchezo kumalizika akiwa nyuma kwa alama tatu, Siakam tena alimzidi Gilgeous-Alexander kwenye ‘rebound’ na kuuweka mpira nyavuni, kupunguza tofauti hadi pointi moja.

Wakati wote ambao Oklahoma ilikuwa bila Chet Holmgren au Isaiah Hartenstein, iliathirika - ilipitwa kwa pointi 7 na kupigwa kwenye rebounds kwa 11-2.


3. Alex Caruso yamkuta

Mojawapo wa matukio ya kufurahisha kwenye mchezo ilikuwa ni sekunde za mwisho za robo ya tatu ambapo T.J McConnell alimchambua mlinzi mahiri Alex Caruso.

Caruso alikuwa akimlinda Siakam kwenye kona, lakini alijaribu kubadili mchezaji ili amkabe Mathurin. McConnell alitambua mapema na kumpasia Siakam aliyebaki peke yake kona kabla Caruso hajamaliza mabadiliko ya nafasi.

Mapema katika robo ya nne, Mathurin alimshinda Caruso mara mbili - tena mara moja kwa mpira wa nje na mara nyingine kwa kupenya moja kwa moja hadi kwenye kikapu.