Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Timu za NBA na thamani 2026

KUZIMIA Pict

Muktasari:

  • Mark Walter amekubali kuiuza Lakers kwa Josh Kushner na Bob Iger, miezi 10 tu baada ya kuinunua klabu hiyo. Mkataba huo utamwezesha mkurugenzi mtendaji wa Guggenheim Partners, ambaye anachunguzwa na serikali ya Marekani kuhusu mikopo iliyotolewa kupitia kampuni zake nyingine, kupata faida ya Dola 2.5 bilioni.

MIAMI, MAREKANI: TIMU za Los Angeles Lakers na Minnesota Timberwolves zinatarajiwa kubadilisha wamiliki katika kipindi hiki cha majira ya joto, ambapo miamala yote miwili inasubiri kupitishwa na bodi ya magavana wa Ligi ya Kikapu Marekani (NBA).

Mark Walter amekubali kuiuza Lakers kwa Josh Kushner na Bob Iger, miezi 10 tu baada ya kuinunua klabu hiyo. Mkataba huo utamwezesha mkurugenzi mtendaji wa Guggenheim Partners, ambaye anachunguzwa na serikali ya Marekani kuhusu mikopo iliyotolewa kupitia kampuni zake nyingine, kupata faida ya Dola 2.5 bilioni. Aliinunua timu hiyo kwa Dola 10 bilioni na amekubali kuiuza kwa Dola 12.5 bilioni.

Huko Minnesota Timberwolves, Marc Stad amekubali kununua hisa za Marc Lore na kuwa mmiliki wa Minneapolis pamoja na Minnesota Lynx ya Ligi ya Mpira wa Kikapu ya Wanawake (WNBA), katika mkataba wenye thamani ya Dola 4.5 bilioni. Hizo ni fedha nyingi zenye tarakimu nyingi, lakini bado siyo kiwango kikubwa zaidi katika ligi hiyo ya Amerika Kaskazini.

KUZIM 01

Kwa mujibu wa jarida la Forbes, Golden State Warriors inaendelea kuwa klabu yenye thamani kubwa zaidi NBA, ikiwa na makadirio ya thamani ya Dola 13.5 bilioni ikiwa ni ongezeko la asilimia 23 ikilinganishwa na mwaka uliopita. Klabu hiyo inayomilikiwa na Joe Lacob na Peter Guber ilipata mapato ya Dola 942 milioni na kurekodi faida ya uendeshaji ya Dola 364 milioni.

Mabingwa watetezi, New York Knicks, wanashika nafasi ya pili mbele ya Lakers. Thamani ya klabu hiyo imeongezeka kwa asilimia 29 na kufikia Dola 12.6 bilioni ikiwa na mapato ya Dola 640 milioni na faida ya uendeshaji ya Dola 140 milioni. Los Angeles Lakers inakamilisha tatu bora, ikiwa na thamani iliyofikia Dola 12.5 bilioni ikiwa ni ongezeko la asilimia 25 ikilinganishwa na mwaka uliopita.

Nje ya klabu hizo tatu za juu, thamani za timu nyingine zinashuka chini ya Dola 10 bilioni; Los Angeles Clippers inashika nafasi ya nne ikiwa na thamani ya takribani Dola 7.8 bilioni, huku Boston Celtics ikikadiriwa kuwa na thamani ya Dola 7 bilioni.

Timu nyingine sita zina thamani inayozidi Dola 6 bilioni ambazo ni Chicago Bulls (Dola 6.7 bilioni), Houston Rockets (Dola 6.6 bilioni), Brooklyn Nets (Dola 6.5 bilioni), Philadelphia 76ers (Dola 6.4 bilioni), Miami Heat (Dola 6.1 bilioni) na Phoenix Suns (Dola 6 bilioni).

KUZIM 02

Kwa upande wa ukuaji wa thamani ukilinganisha na mwaka uliopita, San Antonio Spurs ni miongoni mwa timu zilizopiga hatua kubwa, ikiwa na ongezeko la asilimia 27, jambo lililochangiwa kwa kiasi fulani na kiwango bora kilichoonyeshwa na Victor Wembanyama. Memphis Grizzlies inafunga orodha ya klabu 30 za NBA ikiwa na thamani inayokadiriwa kufikia Dola 4 bilioni na faida ya uendeshaji ya Dola 59 milioni.

NBA inaendelea kukua na kuvutia wawekezaji katika miaka ya hivi karibuni, na Forbes inakadiria kuwa mapato ya ligi hiyo yalikaribia Dola 14 bilioni katika msimu uliopita, huku kukiwa na mipango ya kuongeza timu mpya.

KUZIM 03

Las Vegas na Seattle zikiwa katika orodha ya maeneo yanayoweza kupewa timu mpya, zabuni ya kupata umiliki wa klabu huko Las Vegas inaweza kufikia Dola 9 bilioni au hata bilioni 10, bila kujumuisha gharama za kujenga uwanja mpya.

Hata hivyo, mipango ya ukuaji wa NBA haiishii ndani ya mipaka yake. Mazungumzo yanaendelea kuhusu kuanzisha ligi barani Ulaya, hatua ambayo inaweza kuongeza zaidi mapato katika mfuko wa ligi hiyo ya Marekani.


ORODHA YA KLABU ZENYE THAMANI KUBWA ZAIDI NBA

1. Golden State Warriors (Dola 13.5 bilioni)

2. New York Knicks                     (Dola 12.6 bilioni)

3. Los Angeles Lakers    (Dola 12.5 bilioni)

4. Los Angeles Clippers  (Dola 7.8 bilioni)

5. Boston Celtics                       (Dola 7 bilioni)

6. Chicago Bulls             (Dola 6.7 bilioni)

7. Houston Rockets                    (Dola 6.6 bilioni)

8. Brooklyn Nets                        (Dola 6.5 bilioni)

9. Philadelphia 76ers     (Dola 6.4 bilioni)

10. Miami Heat               (Dola 6.1 bilioni)

11. Phoenix Suns             (Dola 6 bilioni)

12. Toronto Raptors                    (Dola 5.9 bilioni)

13. Dallas Mavericks                   (Dola 5.8 bilioni)

14. Atlanta Hawks                       (Dola 5.75 bilioni)

15. San Antonio Spurs    (Dola 5.6 bilioni)

16. Cleveland Cavaliers   (Dola 5.5 bilioni)

17. Washington Wizards  (Dola 5.2 bilioni)

18. Denver Nuggets                    (Dola 5.15 bilioni)

19. Oklahoma City Thunder          (Dola 4.9 bilioni)

20. Utah Jazz                (Dola 4.75 bilioni)

21. Sacramento Kings     (Dola 4.7 bilioni)

22. Milwaukee Bucks      (Dola 4.6 bilioni)

23. Indiana Pacers                     (Dola 4.55 bilioni)

24. Orlando Magic                      (Dola 4.5 bilioni)

25. Charlotte Hornets    (Dola 4.4 bilioni)

26. Portland Trail Blazers           (Dola 4.3 bilioni)

27. Detroit Pistons                     (Dola 4.2 bilioni)

28. Minnesota Timberwolves       (Dola 4.18 bilioni)

29. New Orleans Pelicans           (Dola 4.1 bilioni)

30. Memphis Grizzlies    (Dola 4 bilioni)