Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Owono avunja ukimya baada ya kifo cha De Miguel

Muktasari:

  • Kupitia ujumbe wake wa hisia, Owono amesema bado anapata wakati mgumu kukubaliana na kilichotokea, huku akituma salamu za pole kwa familia ya marehemu, ndugu, jamaa na wote waliomfahamu.

KIPA wa timu ya taifa ya Guinea ya Ikweta, Jesús Owono, amevunja ukimya kufuatia kifo cha kusikitisha cha mshambuliaji Jesús de Miguel, akieleza kuwa tukio hilo ni miongoni mwa nyakati ngumu zaidi katika maisha yake.

Kupitia ujumbe wake wa hisia, Owono amesema bado anapata wakati mgumu kukubaliana na kilichotokea, huku akituma salamu za pole kwa familia ya marehemu, ndugu, jamaa na wote waliomfahamu.

“Hizi ni siku ngumu zaidi katika maisha yangu. Ni vigumu kupata maneno ya kuelezea, na bado ninapata wakati mgumu kuelewa kila kilichotokea,” alisema Owono.

Aliongeza kuwa, licha ya kufahamu kuwa kutakuwa na mambo mengi ya kushughulikia katika siku zijazo, kwa sasa mawazo yake yote yako kwa marehemu De Miguel na maumivu wanayopitia kutokana na msiba huo.

“Kwa sasa, kwa kweli, siwezi kufikiria jambo lolote zaidi ya Jesús na maumivu tunayopitia,” alisema kabla ya kuhitimisha ujumbe wake kwa maneno: “Pumzika kwa amani, Jesús.”