Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Nyota Cagliaria anusurika kifo

Muktasari:

  • Trepy alisafirishwa kwa helikopta kwenda hospitalini baada ya tukio hilo kutokea katika nyumba moja ya kifahari huko Sardinia Jumapili mchana.

SARDINIA, ITALIA; MSHAMBULIAJI wa Cagliari, Yael Trepy (20), ametoka kwenye koma baada ya madaktari kuondoa mashine ya kumsaidia kupumua, siku mbili baada ya kuokolewa akiwa hajitambui kutoka kwenye bwawa la kuogelea.

Trepy alisafirishwa kwa helikopta kwenda hospitalini baada ya tukio hilo kutokea katika nyumba moja ya kifahari huko Sardinia Jumapili mchana.

Cagliari ilitoa taarifa Jumanne jioni kutoka Hospitali ya Santissima Annunziata Civil, jijini Sassari, ambako mchezaji huyo anaendelea kupatiwa matibabu.

Kwa mujibu wa taarifa hiyo, msaada wa mashine ya kupumua pamoja na dawa za kumlaza ulipunguzwa hatua kwa hatua, hali iliyomwezesha Trepy kuamka kutoka kwenye koma.

Daktari Stefania Milia, mkurugenzi wa Kitengo cha Dharura na Uangalizi Maalumu (ICU) katika hospitali hiyo, alisema Trepy alipozinduka alikuwa ametambua mazingira yake na kuonyesha hali nzuri ya fahamu.

“Baada ya kuamka, mgonjwa alipata fahamu kikamilifu. Anaelewa kinachoendelea, anaweza kushirikiana na madaktari na kwa sasa haonyeshi dalili zozote za wazi za matatizo ya mfumo wa fahamu,” alisema Dk Milia.

Hata hivyo, Trepy bado yuko katika chumba cha uangalizi maalumu na anaendelea kufuatiliwa kwa karibu kiafya pamoja na mfumo wake wa upumuaji.

Taarifa iliyotolewa mapema Jumanne ilisema Trepy hana homa na kwamba uwezo wake wa kupumua umeimarika ikilinganishwa na hali yake mbaya alipowasili hospitalini.

Pamoja na maendeleo hayo, madaktari bado wameendelea kuwa waangalifu kuhusu hali yake.

Kwa mujibu wa taarifa iliyofikishwa na BBC Sport, Trepy alikuwa akiogelea pamoja na marafiki zake na inaaminika alipata matatizo baada ya kufika eneo la bwawa ambalo hakuweza kugusa chini.

Alikuwa ametoka kucheza Coppa Italia

Wachezaji wa Cagliari walikuwa wamepewa mapumziko mwishoni mwa wiki baada ya kuifunga Arezzo kwa bao 1-0 katika mchezo wa Coppa Italia Ijumaa.

Trepy alijiunga na akademi ya Cagliari mwaka 2022, baada ya kuanza safari yake ya soka la vijana katika klabu ya US Creteil-Lusitanos ya jijini Paris, Ufaransa.