Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Nico Williams aipa sharti moja Barcelona

NICO Pict

Muktasari:

  • Nico ambaye siku tano zilizopita aliitarifu Athletic Bilbao, kupitia wakala wake, kuwa hana mpango wa kubakia katika timu na anahitaji kujiunga na Barcelona katika dirisha hili.

BARCELONA, HISPANIA: MBALI ya kukubali na kutamani sana kujiunga na Barcelona, winga wa Athletic Bilbao, Nico Williams ametoa sharti moja kwa mabosi wa timu hiyo kabla hajasaini mkataba.

Nico ambaye siku tano zilizopita aliitarifu Athletic Bilbao, kupitia wakala wake, kuwa hana mpango wa kubakia katika timu na anahitaji kujiunga na Barcelona katika dirisha hili.

Hadi sasa Barcelona tayari imeanza mipango ya kulipa kifungu cha kuvunjia mkataba cha mchezaji huyo ambacho ni Euro 58 milioni.

Kila kitu kinaonekana kuwa katika mstari lakini ripoti za hivi karibuni zinaeleza Nico anataka kuhakikishiwa kwamba Barcelona itaweza kumsajili rasmi katika LaLiga na akacheza, kwani kulipa ada ya uhamisho ni hatua moja, wakati kupata leseni ya kucheza LaLiga ni jambo tofauti.

Hii inatokana na hali ya kiuchumi ya Barca kutoendana na sheria za La Liga za matumizi ya pesa ambazo inazitaka klabu kutumia kwa kile ilichoingiza lakini changamoto kwa mabingwa hao watetezi wa ligi ni kwamba uchumi wao umedorora na wanaandamwa na madeni.

Tukio la Dani Olmo msimu uliopita bado lipo kwenye kumbukumbu za wachezaji na mashabiki. Nico, ambaye anatarajiwa kusaini mkataba hadi mwaka 2031, anataka kupata uhakika wa kuepuka matatizo kama hayo.

Msimu uliopita, Dani Olmo pamoja na Pau Víctor walikumbwa na sintofahamu kuanzia wakati wanasajiliwa na hata katikati ya msimu.

Kwanza kabisa Olmo alianza msimu kwa kuchelewa kwa sababu LaLiga haikuidhinisha usajili wake kwa wakati na ilibidi hadi Christensen kupata jeraha Agosti ndio La Liga ikampa nafasi ya kusajiliwa hadi Desemba 31. Lakini Januari mwaka huu, alikumbana tena na matatizo, akaachwa nje ya kikosi kwa siku kadhaa bila mkataba, huku kukiwa na mvutano mkali kati ya Barca na La Liga kabla ya Baraza la Michezo la Hispania kuingilia kati na akaruhusiwa kucheza.

Nico hataki kupitia hali kama hiyo. Ameweka wazi kwa Bilbao kuhusu nia yake ya kuondoka, lakini pia anataka kuhakikisha kuwa ataweza kucheza msimu ujao bila vikwazo vya sheria hiyo ya masuala ya kifedha.

Rais Joan Laporta alionekana mwenye kujiamini jana wakati wa mashindano ya hisani ya gofu yaliyoandaliwa na Ronald Koeman, ambapo alisisitiza kuwa Barcelona inafuata masharti yote ya LaLiga na Fair Play ili kuwa na uwezo wa kusajili wachezaji katika dirisha hili.

Javier Tebas, rais wa LaLiga, amekumbusha kuwa Barcelona bado haijafikia uwezo wa kumsajili Nico na kumuingiza katika mfumo.