Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

NBA All-Star 2026 inawahusu

Muktasari:

  • Hii itakuwa ni mara ya saba kwa Mchezo wa All-Star kuchezwa katika eneo la mji mkuu wa Los Angeles, mara ya nne kuandaliwa na Clippers na mara ya kwanza kuchezwa Inglewood tangu mwaka 1983.

LOS ANGELES, MAREKANI: NBA All-Star Game ni mchezo wa kila mwaka unaoandaliwa na Chama cha Taifa cha Mpira wa Kikapu Marekani, ukiwakutanisha wachezaji 24 bora wa ligi hiyo. Tangu mwaka 2022, mchezo huu umekuwa ukifanyika Jumapili ya tatu ya Februari, siku ambayo pia huangukia mashindano ya Daytona 500, ambayo kwa kawaida hufanyika wiki moja baada ya Super Bowl.

Februari 15, 2026 ndiyo utachezwa mchezo huo ukiwa ni toleo la 75 na utaandaliwa na Los Angeles Clippers katika Uwanja wa Intuit Dome, uliopo Inglewood, California.

Hii itakuwa ni mara ya saba kwa Mchezo wa All-Star kuchezwa katika eneo la mji mkuu wa Los Angeles, mara ya nne kuandaliwa na Clippers na mara ya kwanza kuchezwa Inglewood tangu mwaka 1983.

Kwa kuzingatia jinsi wachezaji wa NBA wanavyochaguliwa kuwa All-Star na mchakato wa uteuzi si kwa kuangalia kiwango cha uchezaji pekee, hivyo haipaswi kushangaza kuona wachezaji wenye uwezo mkubwa wakikosa nafasi hiyo mara kwa mara.

Kuna makundi matatu tofauti yanayounda vikosi kila msimu, kila moja likitumia vigezo vyake. Wanaoanza (starters) huchaguliwa kwa kura za mashabiki, wachezaji wenzao na vyombo vya habari. Kwa kawaida hawa ni chaguo zilizo wazi, wachezaji 10 kutoka kwenye kundi la labda 12 au 13 bora zaidi.

Nafasi zilizobaki katika vikosi vya Mashariki na Magharibi hujazwa na makocha husika, ambao mara nyingi huangalia rekodi ya ushindi na kushindwa (W-L) ya timu za wachezaji wanaowania kuwa All-Star.

Kisha kuna chaguo za kamishna wa ligi panapotokea majeruhi. Wakati mwingine huchagua mchezaji aliyepata kura nyingi zaidi baada ya starters; wakati mwingine hafanyi hivyo.

Kwa kadri Mchezo wa All-Star unavyoonekana kama mchezo wa mashabiki, bado kuna chaguo za kushangaza kwa wachezaji wapya wanaoingia kila mwaka. Mwaka jana kulikuwa na wachezaji watano wa mara ya kwanza, Victor Wembanyama, Evan Mobley, Cade Cunningham, Jalen Williams na Alperen Şengün. Ni nadra kukosa angalau mchezaji mmoja au wawili wapya.

Hapa kuna orodha ya wachezaji 10 wanaoweza kuonja All-Star Februari mwakani. Watatu walikuwepo msimu uliopita, pamoja na wengine saba wanaoonekana kuwa na uwezo wa kuchukua hatua kubwa kufikia katikati ya msimu.

Kumbuka, hapa inazingatiwa ustahiki wa jumla wa All-Star, bila kurekebisha uwezekano wa muundo wa USA dhidi ya Kimataifa unaozungumzwa kwa All-Star ya 2026. Huo unaweza kupunguza idadi ya nyota wa Marekani na kuongeza wa kigeni, ikilinganishwa na utaratibu wa kawaida wa wawakilishi 12 Mashariki na 12 Magharibi.


1. Chet Holmgren (Oklahoma City Thunder)

Hakuna anayetarajia Shai Gilgeous-Alexander kuondoka kwenye orodha ya Magharibi, lakini kuna mifano mingi ya Oklahoma City kama mabingwa watetezi na washindani wakuu kuongeza All-Star watatu. Holmgren alikuwa karibu mwaka jana; alikosa nafasi hiyo kutokana na uwepo wa wachezaji wengi warefu. Huenda ikahitaji majeruhi kupunguza ushindani unaojumuisha Wembanyama, Şengün, Nikola Jokić, Anthony Davis na Jaren Jackson Jr.

2 & 3. OG Anunoby au Mikal Bridges (New York Knicks)

Hawa wawili walitajwa pia mwaka jana bila kufanikiwa. Kuna nafasi Mashariki, huku nyota kama Jayson Tatum (Boston), Tyrese Haliburton (Indiana) na Damian Lillard (aliyekuwa All-Star na Milwaukee) wakikosekana msimu huu. Changamoto kwa Anunoby na Bridges ni kung’ara vya kutosha nyuma ya Jalen Brunson na Karl-Anthony Towns na kuepuka kugawanya kura kati yao.


4. Franz Wagner (Orlando Magic)

Paolo Banchero aliingia All-Star mwaka 2024; Wagner anaweza kufuata. Alifunga pointi za kutosha (wastani wa 24.2 kwa mechi msimu uliopita) lakini anahitaji kuboresha ufanisi, hasa akipiga 29.5% tu ya mipira ya pointi tatu (7/37 raundi ya kwanza dhidi ya Boston). Wing huyu wa futi 6-10 ana miaka 24.


5. Ivica Zubac (LA Clippers)

Changamoto ya uwepo wa nyota wengi wa kati unaomkabili Holmgren pia unamhusu Zubac. Staa huyu mrefu kutoka Bosnia na Herzegovina amekuwa mashine ya double-double kwa miaka mingi, lakini msimu wa tisa ndipo alipocheza dakika na mechi za kutosha kuonyesha takwimu halisi (pointi kwa mechi 16.8, ribaundi kwa mechi 12.6). Aliongoza ligi kwa ribaundi za kushambulia na kujilinda, na alikuwa All-Defensive Team ya pili.


6. Jamal Murray (Denver Nuggets)

Inaweza kushangaza kwamba Murray hajawahi kuwa All-Star licha ya uwezo wake. CJ McCollum ana misimu 10 ya pointi 20+ bila kuchaguliwa, Murray ana minne. Murray anajulikana kung’aa kwenye playoffs, ana pete ya ubingwa, na amekuwa akicheza sambamba na Jokić ambaye ndiye All-Star pekee wa Denver mara zote. Ikiwa mabadiliko ya kikosi yatazaa matunda, Murray anaweza kujiunga na “Joker.”


7. Jaden McDaniels (Minnesota Timberwolves)

McDaniels na Anthony Edwards wamekuwa pamoja tangu kuwasili Minnesota mwaka 2020. Amekuwa akijionyesha zaidi kwenye mfumo wa kocha Chris Finch, huku akiendelea kuwa mlinzi anayeweza kufunika nafasi yoyote. Aina hii ya mchezaji hupendwa na makocha hasa kama rekodi ya Wolves itakuwa nzuri.

8.Norman Powell (Miami Heat)

Powell amekuwa akipanda kwa muda. Baada ya misimu miwili akipata kura za Sixth Man, alianza mechi zote msimu uliopita na kuvuka wastani wa pointi 20. Kuhamia Miami kunampa nafasi ya kung’ara, huku akionyesha ufanisi wa 41.9% kwenye mipira ya pointi tatu kwa misimu minne mfululizo. Hata hivyo, akiwa na miaka 32, anakaribia rekodi ya Nat 'Sweetwater' Clifton, aliyekuwa All-Star wa mara ya kwanza akiwa na miaka 34.

9&10.Amen Thompson (Houston Rockets) au Ausar Thompson (Detroit Pistons)

Mapacha hawa wapo vizuri, ikiwa mmoja wao ataendeleza kuonyesha uwezo mkubwa katika kushambulia, anaweza kuandamana na All-Star wa timu yake Şengün au Cunningham. Amen tayari aliwahi kucheza All-Star katika mashindano ya Rising Stars, lakini tunazungumzia mechi kuu. Mapacha Dick na Tom Van Arsdale waliwahi kufanikisha hilo pamoja mwaka 1970 na 1971.