Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Hakimi aongoza mauaji akimpiku Eto’o

HAKIMI Pict

Muktasari:

  • Beki huyo wa kulia wa Paris Saint-Germain (PSG) alicheza katika ushindi wa mabao 4-2 wa timu yake dhidi ya Manchester City, Jumatano, Uwanja wa Etihad, na kufikisha mechi 79 katika mashindano hayo, akimpita mshambuliaji wa zamani wa Cameroon, Samuel Eto’o, aliyekuwa na mechi 78.

LONDON, ENGLAND: BEKI Achraf Hakimi anaendelea kuimarisha nafasi yake miongoni mwa nyota wakubwa wa soka barani Ulaya, baada ya kupanda hadi nafasi ya nne kwa wachezaji wa Afrika walioicheza mara nyingi Ligi ya Mabingwa Ulaya.

Beki huyo wa kulia wa Paris Saint-Germain (PSG) alicheza katika ushindi wa mabao 4-2 wa timu yake dhidi ya Manchester City, Jumatano, Uwanja wa Etihad, na kufikisha mechi 79 katika mashindano hayo, akimpita mshambuliaji wa zamani wa Cameroon, Samuel Eto’o, aliyekuwa na mechi 78.

Hakimi, mwenye umri wa miaka 27, na Eto’o pia wanafanana kwa kutwaa mataji matatu ya Ligi ya Mabingwa kila mmoja, idadi inayowafanya kuwa miongoni mwa Waafrika waliofanikiwa zaidi katika historia ya mashindano hayo.

HAKI 01

Katika safari yake ya Ligi ya Mabingwa, Hakimi amezichezea klabu nne ambazo ni Real Madrid, Borussia Dortmund, Inter Milan na PSG, anayoitumikia kwa sasa.

Hata hivyo, bado yuko nyuma ya Waafrika wengine watatu kwa idadi ya mechi katika mashindano hayo. Orodha hiyo inaongozwa na Didier Drogba wa Ivory Coast, aliyewahi kuwa mshambuliaji wa Chelsea, akifuatiwa na Mohamed Salah wa Misri na Michael Essien wa Ghana.

Kwa mujibu wa takwimu zilizotajwa katika taarifa hiyo, Salah anaongoza akiwa na mechi 98, Drogba akifuata kwa 92, huku Essien akiwa na 81. Hakimi anashika nafasi ya nne kwa mechi 79, akifuatiwa na Eto’o mwenye 78.

HAKI 02

Akiwa bado ni mchezaji muhimu katika kikosi cha PSG na mwenye miaka mingi ya kucheza mbele yake, Hakimi ana nafasi ya kuendelea kupunguza pengo dhidi ya vinara hao. Akiendeleza kiwango chake na kucheza mara kwa mara, anaweza kuwania rekodi ya kuwa Mwafrika aliyecheza mechi nyingi zaidi katika historia ya Ligi ya


HAKI 03

GUARDIOLA APIGWA BUTWAA

Kocha Pep Guardiola alionekana kushtushwa na matokeo ya Manchester City dhidi ya Paris Saint-Germain (PSG), baada ya mabingwa hao wa Ufaransa kuibuka na ushindi wa mabao 4-2 katika mchezo wa Ligi ya Mabingwa Ulaya, Uwanja wa Etihad.

Guardiola, aliyewahi kuinoa City kwa miaka 10 na kuipa mataji mbalimbali kabla ya kuondoka Mei, alishuhudia timu yake ya zamani ikipata wakati mgumu baada ya PSG kupata mabao matatu ndani ya dakika 32 za kwanza.

Hali hiyo iliwapa mashabiki wa PSG sababu ya kushangilia kwa dhihaka, wakifanya shangwe maarufu la Poznan linalohusishwa na mashabiki wa City, kwa kugeuzia migongo yao uwanjani na kurukaruka kwa pamoja.

Kocha huyo mwenye umri wa miaka 55 alipigwa picha akiwa ameketi jukwaani, mkono wake ukiwa umefunika mdomo, huku akionekana kushindwa kuamini yaliyokuwa yakitokea uwanjani. Ilikuwa mara yake ya kwanza kurejea Etihad tangu kumaliza kipindi chake cha mafanikio akiwa kocha wa City.

Kabla ya mchezo kuanza, Guardiola alikuwa amepokewa kwa heshima kubwa na mashabiki wa City, waliomchukulia kama mmoja wa makocha bora zaidi katika historia ya klabu hiyo. Hata hivyo, hali ilibadilika haraka baada ya PSG kuanza kuonyesha makali yake.

Desire Doue aliipa PSG bao la kwanza dakika ya 13 kwa shuti la chini lililompita kipa Gianluigi Donnarumma, aliyewahi kuitumikia klabu hiyo ya Ufaransa, kabla ya Ousmane Dembélé kuongeza bao la pili kwa kichwa chini ya dakika mbili baadaye.

PSG iliendelea kuishambulia City na kufunga bao la tatu dakika ya 32, Vitinha akimalizia kwa shuti kali ndani ya eneo la hatari baada ya Warren Zaire-Emery kumtengenezea nafasi kwa mguso wa ustadi.

Bao hilo liliwafanya mashabiki wa PSG waliokuwa ugenini kushangilia kwa nguvu, huku wakigeuza migongo yao kuelekea uwanjani na kurukaruka kwa pamoja kwa mtindo wa Poznan, kitendo kilichoongeza maumivu kwa mashabiki wa City.

PSG hatimaye ilimaliza mchezo kwa ushindi wa mabao 4-2, matokeo yaliyoifanya siku ya kurejea Etihad kwa Guardiola kuwa yenye kumbukumbu tofauti na mapokezi mazuri aliyoyapata kabla ya mchezo.


REKODI ZA MECHI:

Mohamed Salah - 98

Didier Drogba - 92

Michael Essien - 81

Achraf Hakimi - 79

Samuel Eto'o - 78