Nafasi ya dhahabu kwa Arsenal, Man City yaanza kupumulia mashine
Muktasari:
- Licha ya matokeo hayo kuipa nafuu Arsenal, bado kuna hofu kutokana na historia ya Manchester City ya kupindua matokeo mwishoni mwa msimu na kubeba ubingwa. Hata hivyo, safari hii Arsenal inaonekana kuwa imara zaidi na yenye dhamira ya kuhakikisha inatwaa taji hilo baada ya kusubiri kwa muda mrefu.
LONDON, ENGLAND: ARSENAL sasa washindwe wenyewe. Wagonga Nyundo hao wa London wana nafasi kubwa ya kutwaa ubingwa wa Ligi Kuu England (EPL) msimu huu baada ya mpinzani wao wa karibu, Manchester City kutoka sare ya mabao 3-3 na Everton, matokeo yaliyopunguza pengo la pointi hadi tano. Kwa sasa Arsenal ina pointi 76 huku City ikiwa na pointi 71 na mchezo mmoja mkononi.
Licha ya matokeo hayo kuipa nafuu Arsenal, bado kuna hofu kutokana na historia ya Manchester City ya kupindua matokeo mwishoni mwa msimu na kubeba ubingwa. Hata hivyo, safari hii Arsenal inaonekana kuwa imara zaidi na yenye dhamira ya kuhakikisha inatwaa taji hilo baada ya kusubiri kwa muda mrefu.
Sare hiyo imeongeza presha kwa City ambayo sasa inakabiliwa na ratiba ngumu ya mechi zilizobaki. Itaanza kwa kuikaribisha Brentford, kisha kusafiri kucheza na Crystal Palace kabla ya kwenda ugenini kuikabili Bournemouth na kumalizia dhidi ya Aston Villa. Kila mechi ina uzito mkubwa katika mbio za ubingwa.
Kocha wa City, Pep Guardiola, ameonekana kutokupa uzito mkubwa hoja kwamba timu yake ina uwezo wa kurejea kwenye mechi ngumu. Hata hivyo, dhidi ya Everton walionyesha kuyumba kwa muda kabla ya kusawazisha mabao katika dakika za mwisho. Hali kama hiyo pia ilionekana katika mechi zilizopita, ikiwemo ushindi mwembamba dhidi ya Burnley na ushindi wa taabu dhidi ya Southampton kwenye FA Cup.
Kwa upande wa Arsenal, kikosi cha Mikel Arteta kimebakiwa na mechi tatu dhidi ya West Ham United, Burnley na Crystal Palace, ambazo zinaweza kuamua hatima ya ubingwa wao. nal, bado kuna hofu