Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Simeone: Tumebadili hoteli ili kubana matumizi, sio ushirikina

SOMIONE Pict

Muktasari:

  • Atletico Madrid usiku wa leo inashuka uwanjani Emirates kuvaana na Arsenal katika mechi ya mkondo wa pili ya nusu fainali ya Ligi ya Mabingwa Ulaya. Mara ya mwisho timu hiyo ilipotembelea jijini London, Oktoba 2025, ilikubali kipigo kizito cha mabao 4-0 dhidi ya Arsenal.

KOCHA wa Atletico Madrid, Diego Simeone, amepuuza madai kuwa alibadili hoteli ya timu hiyo jijini London kutokana na imani za kishirikina, akisisitiza kuwa uamuzi huo ulilenga kuokoa fedha za klabu.

Atletico Madrid usiku wa leo inashuka uwanjani Emirates kuvaana na Arsenal katika mechi ya mkondo wa pili ya nusu fainali ya Ligi ya Mabingwa Ulaya. Mara ya mwisho timu hiyo ilipotembelea jijini London, Oktoba 2025, ilikubali kipigo kizito cha mabao 4-0 dhidi ya Arsenal.

Kufuatia kichapo hicho, kuliibuka ripoti nchini Hispania kuwa Simeone (56) aliamua kubadili mahali walipofikia safari hii ili kukwepa mkosi. Hata hivyo, Simeone ameweka wazi kuwa sababu kuu ni uchumi.

SIM 01

"Tuko vizuri zaidi kuliko tulivyokuwa mwezi Oktoba na hoteli hii ni ya bei nafuu zaidi. Hiyo ndiyo sababu tulibadili," amesema Simeone akizungumza na waandishi wa habari.

"Tuna imani na kile tunachotaka kukifanya uwanjani, ingawa matokeo hayatategemea sisi pekee. Tumejipanga vyema kwa kile tunachohitaji kufanya," ameongeza.

Timu hizo zitaingia uwanjani zikiwa kumbukumbu ya sare ya 1-1 katika mechi ya mkondo wa kwanza iliyopigwa Riyadh Air Metropolitano jijini Madrid wiki iliyopita. Katika mechi hiyo, mshambuliaji Julian Alvarez alifunga bao la penalti akisawazisha lile la Viktor Gyokeres, ambalo pia lilikuwa la mkwaju wa penalti.

SIM 02

Arsenal inapambana kufika fainali ya michuano hiyo kwa mara ya kwanza tangu mwaka 2006, ikisaka taji la kwanza la Ligi ya Mabingwa. Kwa upande wa Atletico Madrid inatafuta nafasi ya fainali ya kwanza tangu mwaka 2016, baada ya kupoteza fainali mbili za awali dhidi ya wapinzani wao wa jadi, Real Madrid (2014 na 2016).