Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Mukisa, Muhoozi walivyoipa matumaini Uganda

MUKISA Pict

Muktasari:

  • Uganda ilifuzu hatua ya mtoano baada ya kumaliza nafasi ya pili katika kundi B, ikianza kwa kipigo cha mabao 3-0 dhidi ya Korea Kusini, kisha kutoka suluhu na Ecuador kabla ya kufufua matumaini kwa kuichapa New Caledonia mabao 6-0 katika mchezo wa mwisho.

NYOTA wawili wa Uganda, Owen Mukisa na Henry Muhoozi ni miongoni mwa wachezaji waliong’ara katika kikosi cha Uganda, ambacho kimefuzu hatua ya mtoano ya fainali za Kombe la Dunia la vijana chini ya miaka 17 zinazoendelea Doha, Qatar.

Uganda ilifuzu hatua ya mtoano baada ya kumaliza nafasi ya pili katika kundi B, ikianza kwa kipigo cha mabao 3-0 dhidi ya Korea Kusini, kisha kutoka suluhu na Ecuador kabla ya kufufua matumaini kwa kuichapa New Caledonia mabao 6-0 katika mchezo wa mwisho.

Ushindi huo, uliambatana na mchezo mwingine wa kundi hilo baada ya Korea Kusini kuitandika Ecuador ambayo ilikuwa nafasi ya pili mabao 3-2, matokeo hayo yaliifanya Uganda kumaliza nafasi ya pili ikiwa na pointi nne na kufuzu moja kwa moja hatua ya 32 bora.

Mukisa, ambaye ni nahodha wa timu hiyo mwenye umri wa miaka 15 alionyesha ubora wake wa kufunga mabao matatu katika ushindi wa mabao 6-0 dhidi ya New Caledonia.

MUKI 01

“Unapotazama namna Henry anavyocheza, inalingana na mfumo wetu wa uchezaji. Ni kipaji cha ajabu. Nina heshima kubwa sana kwa kijana huyu na mashindano haya yamenifanya nimheshimu zaidi. Najua ana uwezo mkubwa sana wa kufika mbali,” amesema kocha wa Uganda, Kingston Laryea.

“Owen ni mchezaji wa ajabu. Ni kiongozi ndani na nje ya uwanja, na uwepo wake katika timu una uzito mkubwa,” amesema kocha huyo.

Mukisa na Muhoozi walionekana kuwa na furaha kubwa baada ya mchezo dhidi ya New Caledonia. Uganda iliingia katika mchezo huo ikifahamu huenda ilihitaji kufunga mabao mengi ili kupata nafasi ya kuipiku Ecuador iliyokuwa nafasi ya pili katika Kundi B.

“Ulikuwa uzoefu mzuri sana. Ni heshima kwetu kuwa hapa. Ni jambo lisiloaminika kwa nchi kama Uganda kuwa na mchezaji anayeweza kufunga hat-trick katika mashindano haya! Ninalipenda jambo hilo,” amesema Mukisa.

Mechi za Uganda katika Kombe la Dunia la vijana chini ya miaka 17 zimekuwa zikiambatana na shamrashamra na kelele za mashabiki wake wenye nguvu, ambao wamekuwa wakiipa timu hiyo sapoti kubwa muda wote wa mechi.

MUKI 02

Alipoulizwa kwa nini anadhani timu yao imevutia hisia za wananchi wengi nchini Uganda, Mukisa amesema: “Wanapenda aina ya soka tunalocheza. Tunajaribu kutawala kila eneo la mchezo. Iwe katika umiliki wa mpira au mipira ya adhabu, huu ndio mtindo wetu wa kucheza.

“Katika kila mchezo, tunathibitisha jambo jingine jipya. Katika hatua ya mtoano, mnaweza kutarajia kitu tofauti, ambacho kitakuwa cha kuvutia sana.”

Uganda itafahamu mpinzani wake wa hatua ya 32 bora baada ya kukamilika kwa michezo ya makundi Ijumaa. Mchezo huo unatarajiwa kuchezwa Jumatatu au Jumanne.

“Itakuwa mechi ngumu kwetu. Hii ni hatua kubwa, lakini tunapaswa kuingia uwanjani tukiwa na tabia ya ushindani. Tunatamani kushinda,” amesema Muhoozi.

Hii ni mara ya pili mfululizo taifa hilo linacheza hatua ya mtoano baada ya mwaka 2025 kuishia hatua ya 32 bora.