Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

MC Alger yatuma ujumbe Yanga, Simba yatajwa

MC ALGER Pict

Muktasari:

  • Yanga na MC Alger zimepangwa Kundi B pamoja na Zamalek ya Misri na Club Africain ya Tunisia huku kila timu ikihitaji kuanza vizuri ili kujiweka katika nafasi nzuri ya kufuzu hatua inayofuata.

MC ALGER ya Algeria imeweka wazi dhamira yake ya kuanza kwa ushindi katika  hatua ya makundi ya Ligi ya Mabingwa Afrika, ikisema haijasafiri hadi Zanzibar kutafuta sare dhidi ya Yanga, bali kuondoka na pointi zote tatu.

Kauli hiyo imetolewa leo, Ijumaa  na kocha wa muda wa timu hiyo, Karim Delhoum, kuelekea mchezo wa kesho, Jumamosi, Novemba 28, 2026 utakaopigwa kwenye Uwanja wa New Amaan Complex, Zanzibar huku akieleza  kuwa kikosi chake kinafahamu uzito wa mchezo huo na kimejiandaa kupambana.

Yanga na MC Alger zimepangwa Kundi B pamoja na Zamalek ya Misri na Club Africain ya Tunisia huku kila timu ikihitaji kuanza vizuri ili kujiweka katika nafasi nzuri ya kufuzu hatua inayofuata.

"Huu ni mchezo wa kwanza wa hatua ya makundi, tunakutana na klabu kubwa yenye uzoefu wa mashindano haya. Tunajua kinachotusubiri na tunajua tunachopaswa kufanya ili kurudi na pointi nyumbani. Tumekuja hapa kushinda si kwa ajili ya kutafuta sare," amesema Delhoum.

FAD 03

Kocha huyo amesema wanachohitaji kwa sasa ni kuhakikisha wachezaji wake wamepata nafuu ya kutosha baada ya safari na wako tayari kukabiliana na Yanga katika mchezo ambao anaamini utakuwa mgumu kwa pande zote mbili.

Akizungumzia Fadlu Davids, Delhoum amesema anaifahamu vizuri historia ya kocha huyo, hasa kutokana na uzoefu wake wa kuifundisha Simba kabla ya kwenda Morocco msimu uliopita.

Amesema wamefanya uchambuzi wa kutosha kuhusu Yanga na wanaufahamu mfumo wa uchezaji wa Fadlu huku akiamini wapinzani wao nao wamefanya kazi kama hiyo kuichunguza MC Alger.


"Ni kocha tunayemfahamu vizuri. Aliwahi kuifundisha Simba na kufanya vizuri, kisha msimu uliopita alikuwa Morocco. Tunajua namna anavyofanya kazi na tumefanya uchambuzi wa timu yake. Hata wao naamini wametuchambua, hivyo utakuwa mchezo mgumu kwa timu zote mbili," amesema.

Delhoum amesema pamoja na ugumu wa Kundi B, lengo lao la kwanza ni kufuzu hatua inayofuata, akieleza kuwa timu zote nne zilizopo kwenye kundi hilo zina ubora na zina uwezo wa kupambana kupata matokeo.

SIMB 04

Amesema MC Alger haiwezi kujiwekea mipaka kwa kuangalia majina ya wapinzani wake, bali inapaswa kuonyesha ubora wake na kupambana dhidi ya kila timu itakayokutana nayo.

Ameeleza pia kuwa wanaifahamu vizuri nguvu ya soka la Tanzania, akizitaja Yanga, Simba na Azam FC miongoni mwa klabu ambazo zimekuwa zikishiriki mashindano ya Afrika mara kwa mara.

Kwa mujibu wa Delhoum, uzoefu wa klabu hizo katika mashindano ya Afrika unaonyesha ushindani wa soka la Tanzania, hivyo MC Alger inapaswa kuwa tayari kwa changamoto ya mchezo huo.