Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Mtunisia amuweka kando Lorch

Muktasari:

  • Kwa mujibu wa mtandao wa Erem News, kocha huyo raia wa Tunisia amefikia uamuzi huo baada ya kutathmini kikosi chake katika maandalizi ya msimu mpya na kuona kuwa mshambuliaji huyo wa Afrika Kusini, pamoja na wachezaji wengine, hawahitajiki tena.

TRIPOLI, Libya: MSHAMBULIAJI Thembinkosi Lorch ameingia katika wakati mgumu ndani ya klabu ya Al-Ittihad ya Libya baada ya kocha Faouzi Benzarti kuripotiwa kumuondoa kwenye mipango yake kuelekea msimu wa 2026/27 wa Ligi Kuu ya Libya.

Kwa mujibu wa mtandao wa Erem News, kocha huyo raia wa Tunisia amefikia uamuzi huo baada ya kutathmini kikosi chake katika maandalizi ya msimu mpya na kuona kuwa mshambuliaji huyo wa Afrika Kusini, pamoja na wachezaji wengine, hawahitajiki tena.

Ripoti hiyo inaeleza kuwa ujio wa winga wa zamani wa timu ya taifa ya Morocco, Sofiane Boufal, umeongeza ushindani kwa Lorch, kutokana na nyota hao kucheza nafasi zinazofanana.

Hali hiyo imekuwa changamoto zaidi kwa Lorch kutokana na kanuni za Ligi Kuu ya Libya kuruhusu kila timu kusajili wachezaji saba pekee wa kigeni. Benzarti ameripotiwa kuamua kumwacha Lorch nje ya orodha ya wachezaji wa kigeni anaowahitaji kwa msimu ujao.

Lorch, mwenye umri wa miaka 33, alijiunga na Al-Ittihad Februari 2026 akitokea Wydad Athletic Club ya Morocco, ambayo sasa inaripotiwa kutaka kumrejesha mshambuliaji huyo.

Hata hivyo, Wydad inakabiliwa na ushindani kutoka kwa klabu nyingine ya Morocco, MAS Fes, ambayo pia inataka kumsajili mchezaji huyo.

Kwa mujibu wa AfricaFoot, MAS Fes ilianza mawasiliano na wawakilishi wa Lorch miezi kadhaa iliyopita na sasa inatarajia kufikia makubaliano yatakayomwezesha kusaini mkataba wa awali, kabla ya kujiunga na klabu hiyo Januari 2027.

Licha ya nia hiyo, Lorch anaripotiwa kuwa aliwahi kuahidi kutocheza tena katika klabu nyingine ya Morocco baada ya kuondoka Wydad Februari mwaka huu.

Hata hivyo, MAS Fes inaonekana kuendelea kusisitiza katika jitihada zake za kumsajili nyota huyo wa zamani wa Orlando Pirates.