Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Mtukutu Barton kubaki gerezani hadi mwakani

Muktasari:

  • Barton, ambaye anatokea Widnes, Cheshire, aliwahi kucheza Manchester City, QPR, Newcastle United, Rangers, Burnley, Marseille na timu ya taifa ya England. Baada ya kustaafu soka aliingia katika kazi ya ukocha akaifundisha Fleetwood Town na Bristol Rovers.

LIVERPOOL, ENGLAND: KIUNGO mtukutu wa zamani wa kimataifa wa England, Joey Barton, ataendelea kubakia mahabusu hadi kesi yake itakaposikilizwa mwakani baada ya ombi lake la kupewa dhamana kukataliwa na mahakama.

Barton, ambaye anatokea Widnes, Cheshire, aliwahi kucheza Manchester City, QPR, Newcastle United, Rangers, Burnley, Marseille na timu ya taifa ya England. Baada ya kustaafu soka aliingia katika kazi ya ukocha akaifundisha Fleetwood Town na Bristol Rovers.

Mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 44 ambaye maisha yake ya soka yalitawaliwa na kucheza rafu na kupigana viwanjani, alipaswa kufikishwa katika Mahakama ya Crown iliyopo Liverpool wiki iliyopita akikabiliwa na shtaka la kusababisha madhara ya mwili kwa nia ya kumdhuru Kevin Lynch, mwenye umri wa miaka 51, katika Klabu ya Gofu ya Huyton & Prescot, Merseyside, mnamo Machi 8, mwaka huu. Hata hivyo, jana kesi hiyo iliahirishwa na kusogezwa hadi Machi mwakani.

Barton, akiwa amevalia jaketi la kijivu lenye zipu, alisikiliza kesi hiyo kupitia video akiwa katika Gereza la HMP Liverpool, ambapo Jaji David Potter alikataa ombi lake jipya la kupewa dhamana.

Nyota huyo mtukutu enzi zake alitikisa kichwa baada ya jaji kuamuru aendelee kubaki mahabusu hadi kusikilizwa kwa hatua ya maandalizi ya kesi hiyo Desemba 11, mwaka huu. Kesi kamili itaanza Machi 8, 2027, ikiwa ni mwaka mmoja kamili tangu tukio kutokea, iki na maana kuwa mchezaji huyo ambaye alikamatwa muda mfupi baada ya tukio hilo atakuwa ametumia miezi 12 akiwa mahabusu akisubiri kesi.

Barton anatuhumiwa kumshambulia Lynch baada ya wawili hao kunywa pombe pamoja katika klabu hiyo ya gofu.

Lynch, ambaye aliwahi kuwa kocha wa timu ya soka isiyo ya ligi na ni mwanzilishi wa shule maalumu ya elimu ya NexGen Academy, inadaiwa alipata majeraha makubwa kwenye jicho kutokana na shambulio hilo. Wiki iliyopita mahakamani wakili wa Barton aliomba kesi iahirishwe ili mashahidi wapya wanaoweza kuwa na taarifa muhimu watafutwe na kuwasiliana nao, jambo ambalo lilikubaliwa na upande wa mashtaka.

Jaji alisema bado kuna mambo magumu ambayo hayajatatuliwa, jambo lililomaanisha kuwa kesi hiyo isingeweza kuanza Septemba 1 kama ilivyopangwa awali, hivyo alipanga tarehe mpya kuwa Machi 8, 2027.