Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Motsepe: Tunamuunga mkono Inafantino

Rais wa Shirikisho la Soka la Kimataifa (FIFA), Gianni Infantino, wakati akihutubia katika mkutano wa Kimkakati wa Shirikisho la Soka Afrika (CAF) unaoendelea katika mji wa Santa Maria, kwenye Kisiwa cha Sal, Cape Verde.

Muktasari:

  • Shirikisho la Soka Afrika (CAF) limetangaza kuwa vyama na mashirikisho wanachama wake wote  54 watamuunga mkono Gianni Infantino kuwania tena urais wa Shirikisho la Soka la Duniani (FIFA) katika uchaguzi unaotarajiwa kufanyika mwakani.

PRAIA, CAPE VERDE: Shirikisho la Soka Afrika (CAF) limetangaza kuwa vyama na mashirikisho yake wanachama wote 54 watamuunga mkono Rais wa Shirikisho la Soka la Kimataifa (FIFA), Gianni Infantino, katika uchaguzi ujao wa urais wa taasisi hiyo.

Msimamo huo umetangazwa na Rais wa CAF, Patrice Motsepe, wakati wa mkutano wa shirikisho hilo uliofanyika nchini Cape Verde, jana Alhamisi, Oktoba 8, 2026.

Motsepe ameeleza kuwa Afrika itaendelea kumuunga mkono Infantino kutokana na mchango wake katika maendeleo ya soka barani humu.

Uungwaji mkono huo unaimarisha nafasi ya Infantino kuelekea uchaguzi wa urais wa FIFA, unaotarajiwa kufanyika mwakani.

Rais wa Shirikisho la Soka la Kimataifa (FIFA), Gianni Infantino (wapili kulia), akifuatiwa na Rais wa Shirikisho la Soka Afrika (CAF), Patrice Motsepe wakati wa mkutano wa Kimkakati wa CAF unaoendelea katika mji wa Santa Maria, kwenye Kisiwa cha Sal, Cape Verde.

Katika mkutano huo, Motsepe aliwaomba wajumbe kumpigia makofi Infantino, ambaye alipokea pongezi hizo.

Uungwaji mkono wa CAF una umuhimu kwa Infantino kwa kuwa shirikisho hilo lina vyama wanachama 54 kati ya vyama wanachama 211 vya FIFA, hivyo kuwa na idadi kubwa ya kura katika uchaguzi huo.

Infantino amekuwa rais wa FIFA tangu mwaka 2016 na anajiandaa kuwania muhula mwingine wa uongozi.

Rais wa Shirikisho la Soka la Kimataifa (FIFA), Gianni Infantino (wakwanza kulia), pamoja na Rais wa Shirikisho la Soka Afrika (CAF), Patrice Motsepe (wapili kushoto) wakati wa mkutano wa Kimkakati wa CAF unaoendelea katika mji wa Santa Maria, kwenye Kisiwa cha Sal, Cape Verde.

Katika kipindi cha uongozi wake, FIFA imeendelea kufadhili miradi ya maendeleo ya soka kupitia Mpango wa Maendeleo ya Soka wa FIFA, unaolenga kusaidia vyama wanachama kuboresha miundombinu na shughuli za soka.

Hata hivyo, uongozi wa Infantino umekabiliwa na ukosoaji kutoka kwa baadhi ya wadau wa soka kuhusu maamuzi mbalimbali ya kibiashara na uendeshaji wa mashindano.

Uungwaji mkono wa CAF unaongeza nguvu kwa Infantino kuelekea uchaguzi huo, ambao matokeo yake yataamuliwa na kura za vyama wanachama wa FIFA.