Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Viwanja vinne ‘kuwaka moto’ Ligi Kuu Bara

LIGI KUU Pict
LIGI KUU Pict

UHONDO wa Ligi Kuu Bara unaendelea tena leo kwa mechi nne kupigwa kwenye viwanja mbalimbali, huku kila timu ikijipanga vizuri, baada ya kupisha kalenda ya Shirikisho la Soka la Kimataifa (FIFA), lililochukua takribani wiki tatu.


LIGI 06

FOUNTAIN VS JKT TANZANIA

Mechi ya mapema leo saa 8:00 mchana, itapigwa kwenye Uwanja wa Sheikh Amri, Abeid, jijini, Arusha, ambapo Fountain Gate inayoshika nafasi ya 14 na pointi nne, itawakaribisha maafande wa JKT Tanzania iliyo nafasi ya 10 na pointi zake saba.

Fountain inakabiliwa na wakati mgumu baada ya kushinda mechi moja moja kati ya sita iliyocheza, huku ikitoka sare pia moja na kupoteza nne, wakati kwa upande wa JKT TZ imeshinda miwili, sare moja na kupoteza mitatu hadi sasa msimu huu.

LIGI 01

Mara ya mwisho kwa timu hizi kukutana, zilishindwa kutambia baada ya kutoka sare ya mabao 2-2, katika mechi kali na ya kuvutia ya Ligi Kuu iliyopigwa kwenye Uwanja wa Meja Jenerali, Isamuhyo, Mbweni, jijini, Dar es Salaam, Mei 21, 2026.


LIGI 04

MBEYA CITY VS KAGERA SUGAR

Kwenye Uwanja wa Sokoine, Mbeya, itashuhudiwa mechi nyingine saa 10:15 Alasiri ya kuvutia kati ya, Mbeya City dhidi ya Kagera Sugar, inayoingia na benchi jipya la ufundi chini ya Kocha Mkuu, Mrundi Cedric Kaze aliyemrithi, Juma Kaseja.

Kaze aliyewahi kufundisha timu mbalimbali ikiwemo Yanga, amejiunga na timu hiyo akichukua nafasi ya Kaseja aliyeondoka Septemba 21, 2026, baada ya mwenendo usioridhisha wa kikosi hicho katika mechi sita za Ligi Kuu ilizozicheza hadi sasa.

LIGI 05

Katika mechi sita za Kagera haijashinda wowote, baada ya kutoka sare mbili na kupoteza nne, ikiwa nafasi ya 15 na pointi mbili, huku kwa upande wa Mbeya City ikishinda tatu, sare moja na kupoteza mbili, ikishika nafasi ya sita na pointi 10.

Mechi ya mwisho iliyopigwa kwenye Uwanja wa Sokoine, Mbeya, zilitoka sare ya mabao 2-2, Novemba 17, 2022, huku ya Mbeya City yakifungwa na Tariq Seif na Hassan Muhamud, wakati ya Kagera Sugar yalifungwa na Anuary Jabir na Mbaraka Yusuph.

Akizungumza na Mwanaspoti, Kaze alisema kwa siku 10 alizokaa kikosini licha ya mapungufu aliyoona, ila amejitahidi kuyarekebisha na matarajio yake ni kuanza upya Ligi Kuu, akihitaji ushindi ili kurejesha ari, nguvu na morali kikosini.

“Ni mechi ngumu lakini muhimu sana kwetu katika kupambania kupata pointi tatu ambazo zitaturejesha vizuri, tunajua wapinzani wetu wamekuwa bora msimu huu ila tutapambana,” alisema Kaze.

Kwa kupande wake Kocha Mkuu wa Mbeya City, Salum Mayanga alisema licha ya mwanzo mzuri lakini wanaheshimu mabadiliko ya kiufundi yaliyofanywa na Kagera Sugar, hivyo, wataingia katika mechi hiyo kwa nidhamu ya hali ya juu na utulivu mzuri.


LIGI 03

DODOMA JIJI VS SINGIDA BLACK STARS

Mechi nyingine itapigwa kwenye Uwanja wa Jamhuri, jijini, Dodoma, saa 1:00 usiku, ambapo Dodoma Jiji inayoshika nafasi ya saba na pointi 10, itakuwa na kibarua cha kupambana na Singida Black Stars iliyo nafasi ya nne na pointi zake pia 10.

Timu hizo zinatofautiana mabao ya kufunga na kufungwa, ambapo Dodoma Jiji imeshinda tatu, sare moja na kupoteza mbili, huku ikifunga mabao manne na kuruhusu manne, wakati Singida imefunga 13 na kuruhusu tisa, ikishinda mitatu, sare moja na kupoteza miwili.

LIGI 02

Dodoma Jiji inaingia katika mechi hiyo ikihitaji kulipiza kisasi, kwa sababu mara ya mwisho zilipokutana kwenye Uwanja wa Airtel, mjini, Singida, Singida Black Stars, ilibaki nyumbani na ushindi mnono wa mabao 5-0, Juni 17, 2026.


LIGI 07

COASTAL UNION VS AZAM FC

Mechi ya mwisho leo itapigwa saa 3:00 usiku, kwenye Uwanja wa Mkwakwani, mjini Tanga, ambapo Coastal Union inayoshika nafasi ya 11 na pointi saba, itacheza dhidi ya matajiri wa Jiji la Dar es Salaam, Azam FC iliyo nafasi ya tatu na pointi 14.

Katika mechi sita ilizocheza Coastal, imeshinda mbili, sare moja na kupoteza tatu, huku kwa upande wa Azam FC iliyocheza mechi saba hadi sasa, imeshinda nne, ikitoka sare mbili na kupoteza moja, jambo litakaloongeza ushindani kwa timu hizo.

LIGI 08

Azam FC inaingia katika mechi hiyo ikiwa na kumbukumbu nzuri, kwani mara ya mwisho ilipocheza kwenye Uwanja wa Mkwakwani mjini, Tanga ilishinda mabao 2-0, Juni 26, 2026, ya Landry Zouzou na Feisal Salum ‘Fei Toto’.