Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Morocco, Senegal kuna fainali WAFCON

Muktasari:

  • Mechi ya kwanza itawakutanisha Senegal dhidi ya Kenya itakayopigwa Uwanja wa Rabat Olympic Stadium saa 12 kamili jioni na ile ya pili ya wenyeji Morocco dhidi ya Algeria itakayochezwa saa 3 usiku katika Uwanja wa Moulay El Hassan Stadium.

BAADA ya kumalizika kwa mechi za kwanza za makundi ya fainali za Kombe la Mataifa ya Afrika kwa wanawake (WAFCON) kundi A linaingia tena mzigoni kwenye mechi za pili.

Mechi ya kwanza itawakutanisha Senegal dhidi ya Kenya itakayopigwa Uwanja wa Rabat Olympic Stadium saa 12 kamili jioni na ile ya pili ya wenyeji Morocco dhidi ya Algeria itakayochezwa saa 3 usiku katika Uwanja wa Moulay El Hassan Stadium.

Mechi hizo mbili zina ladha na mahitaji tofauti kwani kila timu inahitaji pointi tatu ili kujihakikishia nafasi nzuri.

Hadi sasa Morocco ndio vinara wa kundi hilo ikiwa na pointi tatu sawa na Algeria zikitofautiana kwa idadi ya mabao ya kufunga na kufungwa.

Sasa mechi inayowakutanisha wawili hao inatarajiwa kuwa ya ushindani mkubwa kwani yeyote atakayeshinda itampa nafasi ya kufuzu robo fainali moja kwa moja.

Baada ya Kenya kupoteza mechi ya kwanza kwa mabao 4-0 dhidi ya Algeria wana cha kujiuliza kwa Senegal ambayo nayo inahitaji pointi hizo muhimu.

Morocco ilianza mashindano vizuri baada ya kuichapa Kenya mabao 4-0, huku Algeria nayo ikianza ushindi mnono wa mabao 2-0 dhidi ya Senegal.

Ushindi kwa timu hizo mbili zinazoongoza kundi zitaifanya mojawapo kufuzu robo fainali ila ikitokea sare yoyote itaifanya mechi za mwisho kuamua.

Morocco inaingia kwenye mchezo huo ikiwa na rekodi nzuri nyumbani. Hii ni mara ya pili mfululizo timu hiyo inandaa WAFCON, baada ya kufanya hivyo mwaka 2022 na kuandika historia ya kufika fainali kwa mara ya kwanza.

Morocco ilianza kwa sare dhidi ya Burkina Faso, ikaifunga Uganda na Senegal hatua ya makundi, ikaiondoa Botswana hatua ya robo fainali kwa ushindi wa 2-1, kisha ikaitandika Nigeria kwa mikwaju ya penalti katika nusu fainali kabla ya kupoteza 2-1 dhidi ya Afrika Kusini kwenye fainali.

Safari hiyo iliifanya Morocco iwe taifa la kwanza kutoka Afrika Kaskazini kufika fainali ya WAFCON.

Hata hivyo mabao manne dhidi ya Kenya, yakiwemo mawili ya Nahila Jrandi, yameonyesha kuwa Morocco imejenga kikosi chenye uwezo wa kushambulia na kumiliki mchezo. Ushindi dhidi ya Algeria utaifanya iwe karibu na kutimiza lengo la kwanza la kuvuka hatua ya makundi mbele ya mashabiki wake.

Huu ni usiriki wa saba wa Algeria katika mashindano hayo na zote imekuwa ikishiia hatua ya makundi, ilianza kushiriki WAFCON mwaka 2004, 2006, 2010, 2014, 2018 na 2024.

Wakati vita ya kileleni mwa kundi ikipamba moto, mchezo mwingine kati ya Senegal na Kenya utakuwa wa kuwania pointi tatu muhimu. Timu zote mbili zilianza kwa vipigo na sasa zinahitaji ushindi ili kuendelea kuwa na matumaini ya kufuzu.