Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Mokwena aanza na mrithi wa Mayele Pyramids

MOKWENA Pict

Muktasari:

  • Mokwena hivi karibuni alitangazwa kuwa kocha mkuu mpya wa Pyramids FC, akichukua nafasi ya kocha raia wa Croatia, Krunoslav Jurčić.

INARIPOTIWA kuwa, kocha Rulani Mokwena ameanza kwa kasi harakati za kusaka mshambuliaji katika kikosi chake cha Pyramids FC, kufuatia kuondoka kwa mshambuliaji tegemeo, Fiston Mayele.

Mokwena hivi karibuni alitangazwa kuwa kocha mkuu mpya wa Pyramids FC, akichukua nafasi ya kocha raia wa Croatia, Krunoslav Jurčić.

Hata hivyo, ujio wake umeenda sambamba na kuondoka kwa Mayele, ambaye anatajwa kuwa karibu kukamilisha uhamisho wa kujiunga na vigogo wa Libya, Al Ahli Tripoli.

Kwa mujibu wa taarifa kutoka Al Watan Sport, kumpata mbadala wa Mayele imekuwa moja ya vipaumbele vikubwa vya Mokwena, huku kocha huyo wa Afrika Kusini akiripotiwa tayari kuwa ameliambia benchi la uongozi la Pyramids kwamba anataka usajili huo ukamilike haraka iwezekanavyo.

MOKWE 01

Taarifa hiyo imeongeza kuwa, licha ya kutokuwa na jina maalumu la mchezaji anayemlenga kwa sasa, Mokwena ameomba klabu hiyo imsajili mshambuliaji wa kigeni mwenye uwezo wa kucheza nafasi ya straika badala ya kuchukua mchezaji kutoka Ligi Kuu ya Misri.

Mbali na kutafuta mshambuliaji, kocha huyo wa zamani wa Mamelodi Sundowns, pia ameripotiwa kuomba kusajiliwa kwa beki mwingine wa kati ili kuimarisha safu ya ulinzi ya timu hiyo.

Kocha msaidizi wa Pyramids FC, Mohamed Nagy, hivi karibuni alizungumzia ujio wa Mokwena katika mahojiano na kituo cha MBC Masr, akieleza kuwa kocha huyo ana uzoefu mkubwa katika soka la Afrika na nchi za Kiarabu.

MOKWE 02

Nagy amesema: “Mokwena ana uzoefu katika ulimwengu wa Kiarabu na Afrika kupitia muda wake akiwa na Sundowns na Wydad, pamoja na kufahamu mazingira ya soka la Algeria na Libya.

“Ana tamaa kubwa ya mafanikio, anaelewa vizuri kile kinachohitajika kwake, ana uzoefu mkubwa na ameingia akiwa na hamasa kubwa.”

Mokwena anakabiliwa na jukumu la kujenga upya kikosi cha Pyramids baada ya kuondoka kwa Mayele, ambaye alikuwa mmoja wa wachezaji muhimu zaidi wa timu hiyo katika misimu ya hivi karibuni.

MOKWE 03

Mayele aliyetua Pyramids Julai 30, 2023 akitokea Yanga, Juni 30, 2026 amemaliza mkataba na sasa ni mchezaji huru akikaribia kutimkia Al Ahli Tripoli ya Libya.

Katika misimu mitatu aliyokuwa Pyramids, Mayele amefanikiwa kushinda mataji matano ambayo ni Egyptian Cup (2), CAF Super Cup (1), Ligi ya Mabingwa Afrika (1) na FIFA African-Asian-Pacific Cup (1). Pia amekuwa mfungaji bora wa Ligi ya Mabingwa Afrika msimu wa 2024-2025 alipofunga mabao sita na mfungaji bora wa FIFA Intercontinental Cup    alipofunga mabao matatu msimu wa 2025-2026.