Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Msuva asiwaze kwanza kuvunja rekodi

MSUVA Pict

Muktasari:

  • Sisi tumemzoea Msuva ambaye anaweza kufanya masihara katika sehemu nyingine uwanjani lakini sio akifika kwenye boksi la timu pinzani.

SAIMON Msuva aliyecheza mechi mbili zilizopita za Taifa Stars dhidi ya Guinea Bissau na Madagascar sio yule tuliyemzoea sisi kwakweli.

Sisi tumemzoea Msuva ambaye anaweza kufanya masihara katika sehemu nyingine uwanjani lakini sio akifika kwenye boksi la timu pinzani.

Lakini Msuva tuliyemwona kwenye hizi mechi mbili zilizopita ni mwingine kabisa tofauti na ambaye huwa anatutoa kimasomaso.

Kukosa mabao ya wazi vile tena katika mechi mbili mfululizo lazima kuna namna. Narudia tena Msuva wetu halisi tunamjua bhama hasa akiwa karibu na goli.

Yaani amewafunga makipa wakubwa Afrika kama Denis Onyango wa Uganda na Stanley Nwabali wa Nigeria ndo asiwe na uwezo wa kuwafunga makipa wa Guinea Bissau na Madagascar? Haiwezekani.

Inawezekana Msuva alipania sana kufunga katika zile mechi na hivyo kusababisha yatokee yale yaliyotokea ya kukosa mabao ya wazi ambayo labda yangetubeba Tanzania kwenye kundi letu hivi sasa.

Na kupania huko labda ni kwa sababu amebakisha bao moja tu ili aweke rekodi ya kuwa mfungaji bora wa muda wote wa Taifa Stars ambapo kwa sasa wapo sawa na Mrisho Ngassa wakiwa wamefunga mabao 25 kila mmoja.

Sasa kama ni kweli, kijiwe kinamshauri Msuva katika mechi zinazofuata za Taifa Stars asicheze kwa kuiwaza sana rekodi anayoinyemelea kuweka na badala yake kipaumbele cha kwanza kiwe ni kuisaidia Stars.

Kama aliweza kufunga mabao 25, hatoshindwa kufunga bao moja. Apunguze tu kupania bao litakuja na heshima ataiweka huku akiwa ameisaidia timu.