Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Mohamed Salah akaribia kutua Besiktas

SALAH Pict

Muktasari:

  • Salah, anayejulikana kama Mfalme wa Misri, mwenye umri wa miaka 34, amefikia makubaliano ya kuvunja mkataba wake wa pauni 400,000 kwa wiki mwaka mmoja kabla ya kumalizika.

ISTANBUL, UTURUKI: MWANDISHI maarufu wa masuala ya usajili, Fabrizio Romano, amethibitisha kuwa mazungumzo kati ya Mohamed Salah na klabu ya Besiktas yanaendelea, licha ya klabu hiyo kutoa taarifa ya kupinga kwamba hakuna dili lililokamilika.

Salah, anayejulikana kama Mfalme wa Misri, mwenye umri wa miaka 34, amefikia makubaliano ya kuvunja mkataba wake wa pauni 400,000 kwa wiki mwaka mmoja kabla ya kumalizika.

Baada ya kutofautiana na viongozi wa klabu pamoja na kocha Arne Slot, iliamuliwa kuwa nyota huyo ataondoka na sasa yuko huru kufanya mazungumzo ya kujiunga na klabu nyingine.

Changamoto kwa mshambuliaji huyo ni kwamba hadi sasa hajapokea idadi kubwa ya ofa zenye thamani kubwa kama ilivyokuwa ikitarajiwa.

Nyota wa Liverpool, Mohamed Sala ambaye ametangaza kuondoka Anfield mwishoni mwa msimu huu. Picha na Mtandao

Awali, klabu kubwa za Saudi Arabia zilikuwa tayari kumpa mshahara wa hadi pauni milioni 1.67 kwa wiki, lakini safari hii zimekuwa kimya katika mbio za kumsajili.

Klabu za Marekani zinazoshiriki MLS pia zinamuhitaji Salah, lakini uwezo wao wa kifedha hauwezi kufikia kiwango cha mshahara anaoutaka.

Kwa sasa Besiktas imejitosa kwa nguvu kutaka kumpata nyota huyo.

Klabu hiyo ya Ligi Kuu Uturuki ipo tayari kumpa mkataba wenye thamani ya euro milioni 12 kwa mwaka, sawa na takribani pauni milioni 10 kwa mwaka, kiasi ambacho ni karibu nusu ya alichokuwa akilipwa Liverpool.

SALA 02

Hata hivyo, bado kuna hatua kadhaa za kukamilisha dili hilo, huku Besiktas ikitoa taarifa rasmi ikikanusha kuwa hakuna biashara ya usajili iliyokamilika.

Romano amesema hatua hiyo ni ya kawaida kwa sababu hakuna makubaliano rasmi yaliyowekwa saini.

Amesema:

"Watu wengi wanauliza kuhusu Mohamed Salah, kwa nini Besiktas wamekanusha taarifa hizi."

"Sababu ni kwamba hadi sasa hawajakamilisha dili lake. Mpaka makubaliano yakamilike na kutiwa saini, ni kawaida kwa klabu kuwa makini."

SALA 01

Aliendelea:

"Besiktas ipo kwenye mazungumzo na Mohamed Salah. Mazungumzo yapo na tayari wamemtumia ofa rasmi."

"Lakini kabla ya kusema Salah amesaini, safari imepangwa au amefanyiwa vipimo vya afya, lazima tusubiri makubaliano rasmi."

"Hadi sasa bado tunasubiri hatua zinazofuata kabla ya kusema yeye ni mchezaji mpya wa Besiktas. Tusiwe na haraka."

"Nitatoa taarifa sahihi kwa wakati unaofaa kwa sababu Salah pia ana ofa mezani kutoka MLS na Saudi Arabia, huku Besiktas ikitaka kuhakikisha kwanza imefikia makubaliano kamili na mchezaji."

SALA 02

Inatarajiwa mazungumzo hayo kuendelea tena Jumatatu, hatua inayoweza kuifanya Besiktas kukamilisha moja ya usajili mkubwa zaidi katika historia yake.

Klabu hiyo, ambayo ni nguvu ya tatu katika soka la Uturuki nyuma ya Galatasaray na Fenerbahce, inalenga kujijenga upya baada ya msimu uliopita kuwa wa kiwango cha chini.