Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Mshahara kikwazo Salah kutua Saudia

SALAH Pict

Muktasari:

  • Salah mwenye umri wa miaka 34 kwa sasa ni mchezaji huru baada ya kuondoka Liverpool mwishoni mwa mwezi Juni, akihitimisha safari ya miaka tisa iliyokuwa na mafanikio makubwa ndani ya klabu hiyo.

CAIRO, MISRI: NYOTA wa Misri, Mohamed Salah bado anaendelea na mazungumzo ya kuhamia Ligi Kuu ya Saudi Arabia, lakini mshahara anaouhitaji umeonekana kuwa kikwazo kikubwa katika kufanikisha dili hilo.

Salah mwenye umri wa miaka 34 kwa sasa ni mchezaji huru baada ya kuondoka Liverpool mwishoni mwa mwezi Juni, akihitimisha safari ya miaka tisa iliyokuwa na mafanikio makubwa ndani ya klabu hiyo.

Katika kipindi chake Anfield, mshambuliaji huyo alitwaa mataji mawili ya Ligi Kuu England, Kombe la FA na Ligi ya Mabingwa Ulaya, huku akijijengea heshima kama mmoja wa wachezaji bora kuwahi kuitumikia Liverpool.

SALAH

Kwa muda mrefu Salah amekuwa akihusishwa na uhamisho wa fedha nyingi kwenda Saudi Arabia, huku Al-Hilal na Al-Qadsiah zikitajwa kuwa klabu zenye nafasi kubwa ya kumsajili.

Hata hivyo, taarifa zinaeleza kuwa mazungumzo hayo yamekwama kwa sasa kutokana na viongozi wa klabu hizo kuona kiwango cha mshahara anachohitaji nyota huyo ni kikubwa mno na wanajaribu kushusha gharama za makubaliano hayo.

Inaelezwa kuwa baada ya kusaini mkataba mpya na Liverpool mwezi Aprili 2025, Salah alikuwa akilipwa mshahara wa pauni 400,000 kwa wiki.

Licha ya changamoto hiyo, mazungumzo yanaendelea, huku dili hilo likiwa na uwezekano wa kumkutanisha tena Salah na Michael Edwards, aliyekuwa mkurugenzi wa michezo wa Liverpool na mtu aliyesimamia usajili wake kutoka AS Roma mwaka 2017.

SALA 02

Edwards mwenye umri wa miaka 47, ambaye hivi karibuni ameondoka ndani ya Fenway Sports Group, anaripotiwa kuwindwa na Al-Hilal kwa lengo la kupewa nafasi ya Ofisa Mtendaji Mkuu (CEO).

Kutokana na nguvu yao kifedha, Al-Hilal pamoja na Al-Qadsiah bado wanaonekana kuwa mbele katika mbio za kukamilisha usajili wa Salah wakati ambapo Ligi Kuu ya Saudi Arabia inaendelea kuvutia mastaa wakubwa duniani.

Al-Hilal inaungwa mkono na wawekezaji binafsi wenye uwezo mkubwa wa kifedha, akiwemo bilionea na mwanamfalme Al Waleed bin Talal Al Saud, ambaye ni miongoni mwa watu matajiri zaidi nchini Saudi Arabia.