Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Mo Salah afichua jambo Morocco

SALAH Pict

Muktasari:

  • Misri, inayowania kuvunja rekodi kwa kutwaa taji lake la nane barani Afrika, ilifuzu hatua ya robo fainali baada ya ushindi mgumu wa mabao 3–1 dhidi ya Benin katika muda wa nyongeza.

RABAT, MOROCCO: NAHODHA wa timu ya taifa ya Misri, Mohamed Salah ameshusha presha ya matarajio ya kuonekana kama timu inayopewa nafasi kubwa ya kutwaa ubingwa wa Kombe la Mataifa ya Afrika (AFCON) 2025 huko Morocco.

Misri, inayowania kuvunja rekodi kwa kutwaa taji lake la nane barani Afrika, ilifuzu hatua ya robo fainali baada ya ushindi mgumu wa mabao 3–1 dhidi ya Benin katika muda wa nyongeza.

Salah aliiongoza timu yake kwa mara nyingine tena, akifunga bao la tatu lililohitimisha ushindi huo. Bao hilo limemfanya awe na jumla ya mabao matatu katika mechi tatu alizocheza kwenye mashindano hayo.

“Sidhani kama sisi tunapewa nafasi,” amesema. “Tuna wachezaji wengi vijana, wengi wao wanacheza ligi ya nyumbani Misri. Tunapigania nchi yetu, halafu tutaona tutafika wapi. Kila mmoja hapa anajitahidi kutoa kiwango chake bora.”

Salah ameshiriki katika mechi zote za Misri isipokuwa mechi ya mwisho ya hatua ya makundi dhidi ya Angola, aliyokosa baada ya timu tayari kufuzu.

“Hakuna mechi rahisi Afrika siku hizi kwa sababu viwango vimekaribiana sana. Hakuna timu zinazopigwa mabao manne au matano kirahisi na hilo linaonyesha ushindani ulivyokuwa mkubwa,” aliongeza.

Nje ya uwanja, Salah amekuwa akiepuka sana vyombo vya habari wakati wa kambi ya Misri mjini Agadir, akijikita zaidi kwenye mafanikio ya timu na pia kutimiza ndoto yake binafsi.

Akiwa na umri wa miaka 32, bado anatafuta taji lake la kwanza la AFCON, baada ya kupoteza fainali mbili.

Salah pia yuko karibu kuandika historia. Mabao yake matatu aliyofunga Morocco yamemfikisha kwenye mabao 66 ya kimataifa, yakibaki matatu tu kuvunja rekodi ya kocha wake Hossam Hassan aliyefunga mabao 69 akiwa mchezaji. Hassan anaamini kuwa Salah atavunja rekodi hiyo hivi karibuni.

“Ni mchezaji muhimu sana kwetu na pia kwa klabu yake Liverpool,” amesema Hassan katika mahojiano ya awali.

“Ameonyesha uongozi bora kwenye mashindano haya, akiwaongoza wachezaji vijana na kubeba majukumu. Tuna bahati kuwa naye na naamini ataendelea kufunga mabao.”