Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Misri ya Salah yatinga robo fainali Afcon 2025

MISRI Pict

Muktasari:

  • Fursa za wazi za kufunga zilikuwa chache mjini Marrakech, huku Salah, ambaye bado anasaka taji lake la kwanza la AFCON akiwa na taifa lake, akiwa nje ya mchezo kwa kiasi kikubwa hadi alipofunga bao katika dakika ya 124.

MARRAKECH, MOROCCO: MISRI imefuzu hatua ya robo fainali ya Kombe la Mataifa ya Afrika (AFCON) 2025 baada ya kufunga mabao mawili katika muda wa ziada, likiwemo moja kutoka kwa Mohamed Salah, na hivyo kuichapa Benin 3-1 katika mechi ngumu ya hatua ya 16 bora.

Fursa za wazi za kufunga zilikuwa chache mjini Marrakech, huku Salah, ambaye bado anasaka taji lake la kwanza la AFCON akiwa na taifa lake, akiwa nje ya mchezo kwa kiasi kikubwa hadi alipofunga bao katika dakika ya 124.

Baada ya kipindi cha kwanza kumalizika bila bao, kiungo wa Misri, Marwan Attia alivunja ukimya kwa shuti zuri kutoka nje ya boksi lililotinga kona ya juu ya lango, zikiwa zimesalia dakika 20 za muda wa kawaida.

Benin ilicharuka na kutengeneza nafasi na krosi ya Junior Olaitan ilimchanganya kipa Mohamed El Shenawy na kupangua mpira juu ya mstari wa goli, kabla ya Jodel Dossou kuwahi mpira na kufunga bao la kusawazisha dakika saba kabla ya filimbi ya kumaliza mechi dakika 90.

Kwa timu zote kushindana vikali katika muda wa ziada bila kupata mwanya, haikushangaza kuona mpira wa adhabu ndogo ukiamua matokeo, ambapo shuti la Yasser Ibrahim kutoka karibu na eneo la penalti lilipaa juu ya kipa wa Benin, Marcel Dandjinou aliyekuwa hana msaada na mpira ukatinga nyavuni. Salah kisha akaongeza bao la pili katika dakika hizo 30 za ziada, akipenya kwa kasi na kupiga kwa mguu wake wa kushoto na kufunga kwa ustadi mkubwa baada ya shambulizi hilo la kushtukiza.

Matokeo hayo yanaitoa Benin kwenye mashindano hayo, huku Misri ilikuwa inasubiri mshindi wa mechi ya Ivory Coast na Burkina Faso itakayochezwa Jumanne ili kufahamu itacheza na nani kwenye hatua ya robo fainali huko Agadir, Jumamosi.