Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Messi asikilizia jambo kushiriki Kombe la Dunia 2026

MESSI Pict

Muktasari:

  • Mshambuliaji huyo mwenye umri wa miaka 38, anayekipiga katika klabu ya Inter Miami ya Ligi Kuu ya Soka Marekani (MLS), amekuwa akiibua maswali mengi kwa mashabiki wake ambao wanataka kumuona akicheza fainali hizo zitakazofanyika mwaka 2026 kwenye nchi za Marekani, Mexico na Canada.

Nahodha wa timu ya taifa ya Argentina, Lionel Messi, amevunja ukimya na kueleza kiu yake ya kutaka kuwa sehemu ya kikosi kitakachoshiriki fainali za Kombe la Dunia 2026, lakini amesisitiza kuwa atausikiliza mwili wake kabla ya kuchukua uamuzi wa mwisho.

Mshambuliaji huyo mwenye umri wa miaka 38, anayekipiga katika klabu ya Inter Miami ya Ligi Kuu ya Soka Marekani (MLS), amekuwa akiibua maswali mengi kwa mashabiki wake ambao wanataka kumuona akicheza fainali hizo zitakazofanyika mwaka 2026 kwenye nchi za Marekani, Mexico na Canada.

Messi amesema kila mchezaji anatamani kucheza fainali za Kombe le Dunia kwa sababu ndio mashindano makubwa ya soka, lakini kwa upande wake hana budi kusubiri, na kuona kama mwili wake utamruhusu kuwa sehemu ya kikosi cha Argentina.

ME 01
ME 01

“Ni jambo la kipekee sana kushiriki Kombe la Dunia, na ningependa sana kuwa sehemu ya kikosi cha Argentina mwaka 2026,” amesema Messi, ambaye atafikisha miaka 39, mwezi Juni 2025.

“Sipendi kutoa uhakika wa moja kwa moja kama nitakuwa sehemu ya timu, mimi ni binaadamu na lolote linaweza kutokea, kwa hiyo hali yangu ya kimwili ikiwa safi nitakwenda na wenzangu kama itampendeza kocha.

“Nitaangalia hali yangu nitakapoanza maandalizi ya msimu mpya na Inter Miami mwakani, kuona kama ninaweza kuwa katika kiwango cha juu kabisa, kama ninaweza kuwa msaada kwa timu, kwa taifa, ndipo nifanye uamuzi,” amesema mshindi huyo mara nane wa tuzo ya Ballon d’Or, katika mahojiano na NBC News.

ME 02

Messi, ambaye amecheza soka la kulipwa tangu mwaka 2004, anataka kupata nafasi nyingine ya kung’ara kwenye jukwaa kubwa zaidi la soka duniani.

“Nina hamu kubwa kwa sababu ni Kombe la Dunia. Tumetoka kushinda mwaka 2022, na kuwa na nafasi ya kulitetea tena ni jambo la kuvutia sana, kwa sababu kila mara ni ndoto kucheza na timu ya taifa, hasa kwenye mashindano rasmi,” amesema.

Messi alianzia soka la ushindani Barcelona akiwa na umri wa miaka 17, kisha akajiunga na Paris Saint-Germain mwaka 2021 kabla ya kuhamia MLS mwaka 2023.

Kuhusu maisha yake Marekani, Messi amesema: “Ukweli ni kwamba napenda kila kitu kuhusu kuishi hapa Miami. Nilikaa muda mrefu huko Barcelona, mji ambao ni wa kipekee kwangu, ambako nilikulia na kupata kumbukumbu nyingi nzuri ambazo tunazikosa sana.

“Lakini Miami ni mji unaotuwezesha kuishi vizuri, kufurahia maisha, kuwa watulivu, na kuruhusu watoto kuwa wao wenyewe na kufurahia maisha yao ya kila siku.”

Messi ameichezea timu ya taifa ya Argentina katika mechi 195, na kufunga mabao 114.