Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Lionel Messi bado yupo yupo sana tu

MESSI Pict

Muktasari:

  • Gwiji huyo wa Argentina, Messi amesaini mkataba wa miaka mitatu wa kuendelea kuitumikia Inter Miami na dili hilo lilitangazwa jioni ya Alhamisi.

MIAMI, MAREKANI: SUPASTAA, Lionel Messi amesaini mkataba mpya wa kuendelea kuitumikia Inter Miami kwenye MLS hadi atakapokuwa na umri wa miaka 41.

Gwiji huyo wa Argentina, Messi amesaini mkataba wa miaka mitatu wa kuendelea kuitumikia Inter Miami na dili hilo lilitangazwa jioni ya Alhamisi.

Messi tayari ameshaifungia mara 71 tangu alipotua kwenye kikosi hicho akitokea Paris Saint-Germain mwaka 2023. Ndani ya muda huo, staa huyo wa zamani wa Barcelona, alicheza mechi 82, akiasisti mara 37 na kuna matumaini makubwa ya kunyakua MLS Cup.

Inter Miami ilimaliza nafasi ya tatu kwenye upande wa Eastern Conference baada ya kushinda mechi 19 na kutoka sare mara nane katika mechi 34 ilizocheza.

Messi alifunga mabao 28 na asisti 16 katika mechi 28 na sasa anajiandaa na mchezo wa kuwakabili Nashville kwenye mechi ya mtoano. Inter Miami, ambayo kwa sasa inanolewa na mchezaji mwenzake wa zamani wa Argentina na Barcelona, Javier Mascherano, iliichapa Nashville 5-2 wiki iliyopita na kutengeneza msimu wao kwenye ubora mkubwa.

ME 01

Katika mechi hiyo Messi alifunga hat-trick na yupo kwenye kinyang'anyiro cha kuchaguliwa kuwa MVP wa MLS kwa msimu wa pili mfululizo. Messi atakuwa mchezaji wa kwanza kufanya hivyo.

Mshindi huyo mara nane wa Ballon d’Or ameichezea Inter Miami mechi nyingi kuliko alipokuwa PSG na kuendelea kuvunja rekodi kibao katika kuelekea fainali za Kombe la Dunia 2026.

Licha ya umri wake kuwa mkubwa, Messi bado anatazamwa kama mchezaji muhimu kwenye kikosi cha Argentina kinachonolewa na Lionel Scaloni.