Mechi 10 za moto Knicks wakitetea ubingwa NBA
Muktasari:
- Mabingwa watetezi wanapocheza katika uwanja maarufu zaidi duniani, kila mchezo unastahili kutazamwa, lakini kwa huko Marekani kutakuwa na picha mpya kabisa kutokana na mazingira yaliyopo na namna maisha yalivyokwenda kasi ambapo timu nyingi zimeboresha vikosi.
NEW YORK, MAREKANI: HIZI ndizo mechi 10 bora ambazo unapaswa kuziweka kwenye kalenda yako ya kutazama kwa mabingwa watetezi wa NBA, New York Knicks.
Mabingwa watetezi wanapocheza katika uwanja maarufu zaidi duniani, kila mchezo unastahili kutazamwa, lakini kwa huko Marekani kutakuwa na picha mpya kabisa kutokana na mazingira yaliyopo na namna maisha yalivyokwenda kasi ambapo timu nyingi zimeboresha vikosi.
New York Knicks wanatoka katika moja ya kampeni za mchujo zilizovutia zaidi katika historia ya michezo, na utataka kujua kama mafanikio waliyopata kipindi kilichopita yataendelea. Knicks watakutana na vipimo vigumu mapema na mara kwa mara wanapojaribu kutetea ubingwa.
Hii hapa ni michezo 10 ambayo hupaswi kuikosa katika ratiba ya Knicks ya msimu wa 2026-27, ikiwa imepangwa kwa kufuata mpangilio wa tarehe.
UFUNGUZI DHIDI YA SIXERS
Jumanne, Oktoba 20, Philadelphia 76ers watawakaribisha Knicks, na kwa mara ya kwanza katika miaka 53, mabingwa watainua bango kwenye dari maarufu la Madison Square Garden. Baada ya hapo wataanza safari ya kutetea taji dhidi ya timu ambayo huenda ikawa yenye vipaji vingi zaidi katika Kanda ya Mashariki. Mchezo wa Knicks dhidi ya Sixers unaonekana kuwa miongoni mwa mechi kubwa zaidi Mashariki.
MAPEMA TU NA CELTICS
Ijumaa, Oktoba 23, Knicks itakuwa nyumbani kuwakarisha Boston Celtics, ambao wamekuwa timu bora zaidi katika ligi hiyo katika kipindi cha miaka 10 iliyopita na ni timu pekee ya Mashariki yenye rekodi bora za ushindi dhidi ya Knicks (12-11, ikiwamo michezo ya mchujo) katika misimu minne ya Jalen Brunson huko New York. Hata hivyo, tangu walipokutana katika nusu fainali ya Kanda ya Mashariki 2025, Knicks wameshinda michezo saba kati ya 10 iliyopita dhidi yao. Hawa ni wapinzani wawili watakaofungua mchezo wa kwanza wa msimu maarufu wa Prime wenye michezo miwili kwa siku.
MDOMONI MWA PISTONS
Wiki inayofuata yaani Jumanne, Oktoba 27, Detroit Pistons watawakaribisha mabingwa hao. Kama wangekutana katika mechi za mchujo msimu uliopita, huenda mambo yangekuwa tofauti kwa Knicks, kwani Pistons waliwazidi ujanja wakishinda michezo yote mitatu kwa wastani wa pointi 28 wakiwa na mashambulizi bora zaidi pamoja na ulinzi mzuri zaidi dhidi ya Knicks. Ni kutokana na hali hiyo kila shabiki wa kikapu atataka kuona timu hizo zikikutana tena katika kile kinachoweza kuwa ushindani mkubwa kwa miaka michache ijayo.
FAINALI MASHARIKI?
Jumamosi, Novemba 7, Knicks itakipiga na Cleveland Cavaliers. Itakumbukwa kwamba Knicks waliichapa Cavaliers katika fainali za Mashariki, wakishinda michezo yote minne kwa wastani wa pointi 19.3, ukiwamo mmoja ambao walikuwa nyuma kwa pointi 22 katika robo ya nne. Hata hivyo, kulikuwa na ukweli katika kauli ya kocha wa Cavaliers, Kenny Atkinson, kuhusu faida yao katika uchambuzi wa takwimu, kwani walikuwa na ubora zaidi wa nafasi za kufunga kwenye mfululizo huo. Lakini, walishindwa kutumia nafasi vizuri, huku Knicks wakiwa katika kiwango bora. Michezo yao minne ya mapema msimu huu itakuwa nafasi kwa Cavaliers kuthibitisha kwamba wako katika kiwango cha Knicks.
BATO DHIDI YA PACERS
Ijumaa, Novemba 13 itakuwa miongoni mwa mechi bab’kubwa ambapo Knicks watawavuta nyumbani Indiana Pacers. Kumbuka kwamba Knicks ni mabingwa watetezi, lakini safari zao mbili zilizopita katika mchujo zilimalizika kwa kufungwa na Pacers, ambao wamerudi wakiwa na nguvu zaidi baada ya kucheza msimu mzima bila Tyrese Haliburton. Mchezo wao wa kwanza msimu huu utakuwa wa NBA Emirates Cup.
GIANNIS NA HEAT MZIGONI
Kabla ya wikiendi ya mwisho wa Novemba siku ya Ijumaa, Novemba 27 mabingwa watetezi watakaribishwa na Miami Heat jijini Miami.
Knicks dhidi ya Heat ni miongoni mwa mechi kubwa za ushindani zaidi katika kipindi cha miaka 30 iliyopita, na msimu mpya wa ushindani unaanza msimu huu baada ya Giannis Antetokounmpo, ambaye ameshinda michezo 29 kati ya 43 dhidi ya Knicks katika maisha yake NBA akiwa amehamia Miami. Huo utakuwa mchezo wa nne kati ya mitano ya Knicks kucheza nyumbani kwa siku tisa, ikiwa ni mfululizo mrefu zaidi wa michezo ya nyumbani kwao msimu huu.
MARUDIANO FAINALI
Ijumaa, Desemba 25, mwaka huu itaialika San Antonio Spurs na huu utakuwa mwaka wa sita mfululizo kwa Knicks kuandaa mchezo wa saa sita mchana Siku ya Krismasi, na ‘wa marudiano’ ya fainali ambao bila shaka utakuwa na mvuto mkubwa zaidi kati ya michezo hiyo sita. Fainali hizo zilikuwa mfululizo wa pili pekee wa michezo ya mchujo katika kipindi cha miaka 30 ambayo takwimu za mchezo kwa mchezo zinapatikana, ambapo timu iliyoshinda iliweza kugeuza matokeo baada ya kuwa nyuma kwa zaidi ya pointi 10 katika kila moja ya ushindi wake minne.
MIKONONI MW, NUGGETS
Mara tu baada ya sikukuu ya mwaka mpya yaani Jumamosi, Januari 2, 2027, Knicks wataikaribisha Denver Nuggets, ambapo baada ya Nikola Jokic kushinda michezo 13 kati ya 14 ya kwanza aliyocheza dhidi ya Knicks katika maisha yake ya NBA, ameshinda mmoja tu kati ya saba iliyopita, huku akitupia kwa usahihi wa mitupo miwili ya three point kati ya 20 katika michezo miwili waliyopoteza msimu uliopita. Hata hivyo, bado ni mchezaji mwenye changamoto kubwa zaidi ya kumzuia mmoja mmoja katika ligi, na Knicks hawana tena mwamba kama Mitchell Robinson anayeweza kutumia dakika kadhaa kumkabili MVP huyo mara tatu.
LAKERS MWISHO WA MWEZI
Jumamosi, Januari 30, Los Angeles Lakers wataikaribisha Knicks, ambapo mchezo unaofahamika kama NBA Rivals Week unaofadhiliwa na AWS, kati ya timu mbili maarufu zaidi katika ligi pia utawakutanisha Jalen Brunson na mchezaji ambaye aliwahi kucheza nyuma yake huko Dallas, Luka Doncic. Brunson na Doncic wamekutana mara nne tangu Brunson ahamie Knicks, huku ushindi pekee wa Knicks katika michezo minne ukipatikana Februari iliyopita. Brunson alitupia mara nne kati ya 15, lakini alitoa asisti 13 na kufanya kosa moja tu la kupoteza mpira.
MABINGWA WA MWISHO
Siku ya saba ya mwezi wa pili yaani Jumapili, Februari 7, Knicks wataialika Oklahoma City Thunder, ambapo mabingwa wawili wa mwisho wa waliopokezana ubingwa wa NBA watakuwa uwanjani. Mechi hiyo huenda ikatuonyesha timu ambazo huenda pia zikawa zinazopigiwa upatu zaidi wa kubeba ubingwa. Mara hii watakuwa wanakutana kwa mara ya kwanza mwishoni mwa wiki ya 16. Knicks wamepoteza michezo sita iliyopita dhidi ya Thunder, na 17 kati ya 20 ya mwisho, huku wakifunga wastani wa pointi 104.7 kwa kila nafasi 100 za kumiliki mpira katika michezo miwili dhidi yao msimu uliopita.