Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

KASHUKA! Vini Junior mambo si mambo Real Madrid

VINI Pict

Muktasari:

  • Vinicius, mshambuliaji wa kimataifa wa Brazil ambaye alikuwa miongoni mwa waliokuwa wakipewa nafasi kubwa ya kushinda tuzo ya Ballon d’Or mwaka 2024, hapo kati alivunja rekodi ya thamani akifikia Pauni 200 milioni baada ya kuwa sehemu muhimu ya mafanikio ya Real Madrid, ikiwemo ushindi wa Ligi ya Mabingwa Ulaya. Hata hivyo, tangu wakati huo kiwango chake kimeendelea kushuka.

MADRID, HISPANIA: ACHANA na kadi nyekundu aliyolimwa Vinicius Junior dhidi ya Villarreal baada ya kumvuta nywele bila sababu kiungo Nathan Saliba, nyot huyo anakabiliwa na kipindi kigumu ndani ya Real Madrid, huku kiwango chake kikishuka na thamani yake ya soko kuporomoka kwa Pauni 70 milioni ndani ya miezi 18.

VIN 03

Vinicius, mshambuliaji wa kimataifa wa Brazil ambaye alikuwa miongoni mwa waliokuwa wakipewa nafasi kubwa ya kushinda tuzo ya Ballon d’Or mwaka 2024, hapo kati alivunja rekodi ya thamani akifikia Pauni 200 milioni baada ya kuwa sehemu muhimu ya mafanikio ya Real Madrid, ikiwemo ushindi wa Ligi ya Mabingwa Ulaya. Hata hivyo, tangu wakati huo kiwango chake kimeendelea kushuka.

Katika mechi saba za Ligi Kuu Hispania (LaLiga) msimu huu, amefunga bao moja na kutoa pasi tatu za mabao. Kiwango chake duni pamoja na mchezo mbaya dhidi ya Atletico  Madrid, kimeongeza ukosoaji kutoka kwa mashabiki.


VIN 01

USHINDANI NA MBAPPE

Kuwasili kwa Kylian Mbappe kumeongeza ushindani katika safu ya ushambuliaji ya Real Madrid na kumfanya Vinicius kupoteza nafasi yake kama nyota mkuu wa timu. Real Madrid iliwahi kufikiria kumuuza Vinicius, huku Arsenal ikiwa miongoni mwa klabu zilizokuwa zikimfuatilia.

Hata hivyo, pande hizo zilifikia makubaliano ya mkataba mpya utakaomuweka Madrid hadi 2032.

Licha ya mkataba huo, kiwango chake hakijaimarika. Tathmini mpya ya Transfermarkt sasa inampa thamani ya Pauni 130 milioni, kiwango chake cha chini zaidi katika miaka mitatu.

Mratibu wa thamani za soko la wachezaji wa Transfermarkt, Tobias Blaseio anasema Vinicius yupo mbali na kiwango alichowahi kuwa nacho katika miaka yake bora ya soka. “Kwa upande wa uchezaji, amekosa ile nguvu na ubunifu aliokuwa nao awali. Ukosoaji umeenea, na hata mkataba mpya haujaonekana kubadili mwenendo huu,” anasema Blaseio.


VIN 02

ARSENAL BADO NI CHAGUO

Real Madrid bado inaamini Vinicius anaweza kurejea katika kiwango chake bora, lakini mazingira ya klabu hiyo yanaweka presha kubwa kwa wachezaji wanaoshindwa kutimiza matarajio.

Mahitaji yake makubwa ya mshahara yanazifanya idadi ya klabu zinazoweza kumsajili kuwa chache.

Arsenal, ambayo tayari ilionyesha nia ya kumsajili, inaweza kuwa miongoni mwa chaguo endapo Real Madrid itaamua kumuuza.

Kwa sasa, Madrid inatarajia Vinicius ayarejea kwenye kiwango chake na kuthibitisha tena kwa nini aliwahi kutajwa miongoni mwa wachezaji bora zaidi duniani.