Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Mayweather: Sikieni, narudi ulingoni jumla jumla

MAYWETHER Pict

Muktasari:

  • Katika taarifa yake, bingwa huyo mwenye umri wa miaka 48 anadai kuwa atatoka rasmi kustaafu kufuatia pambano lake la maonyesho dhidi ya Tyson litakalofanyika Aprili 25 litakalopigwa huko Kinshasa, DR Congo.

FLORIDA, MAREKANI: BONDIA wa ngumi za kulipwa aliyetangaza kustaafu miaka michache iliyopita, Floyd Mayweather Jr ametangaza kurejea kwa kushtukiza kwenye ndondi za kulipwa baada ya pambano la maonyesho dhidi ya Mike Tyson.

Katika taarifa yake, bingwa huyo mwenye umri wa miaka 48 anadai kuwa atatoka rasmi kustaafu kufuatia pambano lake la maonyesho dhidi ya Tyson litakalofanyika Aprili 25 litakalopigwa huko Kinshasa, DR Congo.

“Naamini bado nina uwezo wa kuweka rekodi zaidi katika mchezo wa ndondi. Kuanzia tukio langu lijalo na Mike Tyson hadi pambano langu lijalo la kulipwa baada na hapo. Hakuna (bondia) atakayevutia mapato makubwa ya tiketi, hadhira kubwa zaidi duniani na fedha nyingi kama matukio yangu,” anasema Mayweather maarufu kama Mr Money.

Mr Money pia alithibitisha kuwa kurejea kwake kutakuwa kwa ushirikiano na CSI Sports ambayo inaendesha vyombo vya habari inayozalisha, kusambaza na kurusha maudhui ya michezo ya mapigano kupitia mtandao wa televisheni wa saa 24 wenye watazamaji zaidi ya milioni 90 duniani.

Waanzilishi wenza wa kampuni hiyo, Richard na Craig Miele, wanasema kusainiwa kwa Mayweather ni ishara kwamba wapiganaji wakubwa zaidi wenye hadhira za kimataifa wanaanza kurejea ulingoni kutoka katika maficho ya ustaafu.

Rejea ya Mayweather kwenye ndondi za kulipwa imepangwa kufanyika majira ya kiangazi mwaka huu dhidi ya mpinzani ambaye bado hajatangazwa.

Mmarekani huyo hajapigana pambano la kulipwa tangu alipomshinda kwa TKO nyota wa mchezo wa ngumi za mapigano ya mateke, Conor McGregor, Agosti 2017 ushindi uliomfanya kufikisha rekodi ya mapambano 50 bila kupoteza.

Inaripotiwa kuwa mbabe huyo wa ngumi alipata zaidi ya Dola 300 milioni kutokana na pambano hilo ambalo pia alitangaza kuwa la mwisho katika taaluma yake ya masumbwi ya kulipwa.

Tangu hapo ameshiriki mapambano ya maonyesho dhidi ya Logan Paul, Tenshin Nasukawa na Aaron Chalmers.  Pambano dhidi ya Chalmers likiwa la kwanza kwake kupigana nchini Uingereza.

Kwa sasa jina ambalo linaweza kujitokeza kama mpinzani wake ajaye ni aliyewahi kuwa mpinzani wake wa zamani, Manny Pacquiao. Wawili hao walizichapa Mei 2015 ambapo Mayweather alishinda kwa uamuzi wa majaji.

Pacquiao naye alistaafu 2021 kabla ya kurejea Julai 2025 kupigana na Mario Barrios. Licha ya kuwa hakupigana kwa karibu miaka minne na akiwa na umri wa miaka 46, Pacquiao alionyesha kiwango bora huku pambano lao la ubingwa wa WBC uzito wa welter likimalizika kwa sare ya majaji wote watatu.