Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Canelo awapiku Messi, LeBron

CANERO Pict

Muktasari:

  • Katika vita ya utengenezaji fedha kwa mwaka huo tu bila kujali kama mtu aliuanza akiwa hana kitu, wapo waliofanya maajabu wakibuna mapato makubwa.

LONDON, ENGLAND: ACHANA na masuala ya viwanjani pamoja na ulingoni, lakini mwaka 2025 ulikuwa na mtifuano mwingine wa namna ya wanamichezo bora duniani kutengeneza fedha na wengine kuongeza utajiri walionao.

Katika vita ya utengenezaji fedha kwa mwaka huo tu bila kujali kama mtu aliuanza akiwa hana kitu, wapo waliofanya maajabu wakibuna mapato makubwa.

Katika orodha ya wanamichezo waliopata mapato makubwa zaidi baada ya mwaka wa fedha wa 2025 uliokuwa na pesa nyingi kwenye michezo huwezi kuacha kulitaja jina la bondia Canelo Alvarez.

CANE 03

Ingawa mwaka huo hakuwa mzuri sana kwake katika ndondi, lakini ulikuwa mzuri kifedha kwani akaunti yake ya benki ilinona. Nyota huyo wa ngumi wa Mexico alivuna Dola 137 milioni mwaka jana pekee na kumuweka katika nafasi ya pili kwenye orodha ya wanamichezo waliolipwa zaidi iliyoandaliwa na Sportico.

Canelo alizidiwa na supastaa wa soka Cristiano Ronaldo wa Al-Nassr pekee aliyekunja Dola 260 milioni, huku Lionel Messi, staa mwingine wa soka anayekipiga Inter Miami ya Marekani akiwa nyuma yake akivuna Dola 130 milioni.

Kwa maana nyingine Canelo alimzidi Messi kwa Dola 7 milioni.

Kwa mujibu wa taarifa mwaka jana Canelo alipigana mapambano mawili dhidi ya William Scull aliyemshinda kwa uamuzi wa majaji wote mwanzoni mwa 2025.

CANE 02

Kisha alizichapa na Terence Crawford akipoteza pambano hilo kwa pointi Septemba 2025. Kwa ujumla Canelo alipata Dola 137 milioni ambapo 125 milioni zilitokana moja kwa moja na mapambano ya ndondi, huku 12 milioni zikitokana na mikataba ya matangazo.

Katika orodha ya wanamichezo kwa ujumla waliovuna mkwanja wa maana ukiwaondoa Ronaldo na Messi, supastaa wa Ligi ya Kikapu Marekani anayekipiga LA Lakers, LeBron James aliondoka na Dola 128.7 milioni huku nahodha wa Al-Ittihad ya Ligi Kuu Saudi Aarabia, Karim Benzema akipata Dola 115 milioni. Hata hivyo, wote hao hawakumfikia Canelo kutokana na mapato makubwa aliyopata.

CANE 01

Ukiondoa mkwanja mrefu aliovuna Canelo mwaka jana pamoja na utajiri wake wa jumla wa Dola 300 milioni, kumbuka kwamba kuna mabondia waliokuja pesa za maana nje ya ulingo wakiongozwa na Mayweather Jr mwenye utajiri wa jumla wa Dola 400 milioni. Mapato yake ya zaidi ya Dola 1 bilioni na utajiri wa takribani Dola 400 milioni vinamfanya kuwa bondia tajiri zaidi kuwahi kutokea duniani.

Wanaomfuatia ni George Foreman (Dola 300 milioni), Manny Pacquiao (Dola 220 milioni), Oscar De La Hoya (Dola  200 milioni), Tyson Fury (Dola 160 milioni), Anthony Joshua (Dola 150 milioni), Lennox Lewis (Dola 140 milioni), Oleksandr Usyk  (Dola 120 milioni) na Sugar Ray Leonard (Dola 120 milioni).