Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Max Dowman avunja rekodi

MAX Pict

Muktasari:

  • Dowman mwenye umri wa miaka 16, aliweka rekodi hizo msimu uliopita, wakati kocha wa Arsenal, Mikel Arteta, alipokuwa akimpa nafasi taratibu katika kikosi cha kwanza.

LONDON, ENGLAND: NYOTA chipukizi wa Arsenal Max Dowman ametunukiwa rekodi tatu za dunia za Guinness kufuatia msimu wake wa kuvutia katika kikosi cha kwanza.

Dowman mwenye umri wa miaka 16, aliweka rekodi hizo msimu uliopita, wakati kocha wa Arsenal, Mikel Arteta, alipokuwa akimpa nafasi taratibu katika kikosi cha kwanza.

Mwezi Novemba mwaka jana, Dowman aliweka historia kwa kuwa mchezaji mwenye umri mdogo zaidi kucheza mechi ya Ligi ya Mabingwa Ulaya baada ya kuingia kama mchezaji wa akiba dhidi ya Slavia Prague.

Wakati huo alikuwa na umri wa miaka 15 na siku 308, akivunja rekodi iliyokuwa inashikiliwa na Youssoufa Moukoko wa Borussia Dortmund kwa tofauti ya siku 75.


MA 03

AANDIKA HISTORIA

Mshambuliaji huyo pia aliingia katika vitabu vya historia vya Premier League baada ya kuwa mfungaji mwenye umri mdogo zaidi katika historia ya mashindano hayo.

Dowman alifunga bao katika ushindi wa Arsenal wa 2-0 dhidi ya Everton mwezi Machi, akiwa na umri wa miaka 16 na siku 73.

Rekodi hiyo ilikuwa ikishikiliwa kwa muda mrefu na James Vaughan, ambaye alikuwa na miaka 16 na siku 271 alipofunga Everton dhidi ya Crystal Palace mwaka 2005.

Cha kuvutia zaidi ni kwamba katika mechi hiyo ya mwaka 2005, kocha wa sasa wa Arsenal, Arteta, alikuwa miongoni mwa wachezaji wa Everton.

MA 02

Baada ya mafanikio hayo, Dowman alikabidhiwa rasmi vyeti vitatu vya 'Guinness World Records' katika hafla iliyofanyika kwenye klabu ya Arsenal.

Pia alikabidhiwa kitabu kipya cha Guinness World Records Football Edition 2027, ambacho kinamuweka kama mchezaji wa kwanza kutajwa katika sehemu maalumu ya kizazi cha Class of '27.

Tom Beckerlegge, mhariri mkuu wa Guinness World Records Football Edition 2027, amesema Dowman ni mchezaji mwenye umri mdogo zaidi katika orodha hiyo na anawakilisha kikamilifu kizazi kipya cha soka.

“Kufikia rekodi tatu za Guinness World Records kabla hata ya kutimiza miaka 17 ni jambo la kipekee.”

MA 01

Beckerlegge aliongeza kuwa soka linaendelea kubadilika, huku rekodi zikiendelea kuvunjwa na vipaji vipya vikizaliwa kila msimu.

Mbali na Dowman, wachezaji wengine waliotajwa katika Class of '27 ni pamoja na Lamine Yamal, Jude Bellingham, Cole Palmer, Erling Haaland na Kylian Mbappe.

Kwa Dowman, mafanikio hayo yanaendelea kumtambulisha kama mmoja wa vipaji vinavyoangaliwa kwa karibu katika kizazi kipya cha soka la dunia.