Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Hatimaye Selena Gomez kanasa kwenye ulimbo!

Muktasari:

  • Selena ambaye ndiye staa wa kike mwenye wafuasi (followers) wengi zaidi katika mtandao wa Instagram duniani, tangu ameolewa na mtayarishaji muziki, Benny Blanco maisha yake yamepata utulivu mkubwa.

Staa wa filamu na muziki kutokea Marekani, Selena Gomez, 34, baada ya kupitia panda shuka nyingi katika maisha yake ya mahusiano, hatimaye sasa ametulia katika chaka lake, sehemu ambayo ni wazi kuwa moyo wake umeridhika.

Selena ambaye ndiye staa wa kike mwenye wafuasi (followers) wengi zaidi katika mtandao wa Instagram duniani, tangu ameolewa na mtayarishaji muziki, Benny Blanco maisha yake yamepata utulivu mkubwa.

Katika umaarufu wake, Selena amekuwa na uhusiano rasmi na wanaume wanne, mwaka 2008 alikuwa na Nick Jonas, kuanzia Desemba 2010 hadi Machi 2018 alikuwa katika uhusiano tena na wa mbali na mwimbaji wa Canada, Justin Bieber.

Mwaka 2015 akawa na DJ Zedd mwenye asili ya Urusi na Ujerumani, uhusiano huu ulikuja muda mfupi baada ya kurekodi wimbo, I Want You to Know (2015). Baada ya kuachana akawa na msanii mwingine wa Canada, the Weeknd waliyedumu kuanzia Januari 2017 hadi Septemba 2017.

Baada ya mpenzi wake wa zamani, mwanamuziki Justin Bieber kuwa na uhusiano na mke wake wa sasa, Hailey, Selena alipitia kipindi kigumu kwa sababu mashabiki wengi walimkosoa mtandaoni wakimuona kama mtu aliyepoteza.

Selena na Bieber ilikuwa ‘kapo’ changa ya vijana ambayo mashabiki wengi waliamini ingefika mbali lakini mambo hayakuwa kama ilivyotarajiwa na wengi. Basi mwisho wa siku wakagawana fito za nyumba ambayo walishaanza kuijenga na kila mmoja akashika njia yake.

Desemba 2023, zikaibuka tetesi zilizodai kuwa Selena na uhusiano na Benny Blanco ambaye ni rafiki Bieber, na haikuchukua muda mrembo huyo akathibitisha jambo hilo kupitia Instagram ambapo ana wafuasi zaidi ya milioni 400

Uthibitisho huo ulikuja baada Selena kutoa maoni yake katika post ya shabiki yake, Popfaction aliyeripoti kuwa mrembo huyo yupo katika uhusiano baada ya kuwa single kwa miaka mingi.

Selena, mkali kibao cha Calm Down (2022) akishirikiana na Rema wa Nigeria, aliandika “ni kweli” kwenye post hiyo, huku akipenda (like) picha iliyokuwa na maelezo kuwa; Inasemekana kuwa Selena Gomez ni mchumba wa Mtayarishaji Benny Blanco.

Licha ya kutangaza hadharani uhusiano wao mwishoni mwa 2023, wawili hao walikuwa wamefahamiana kwa miaka kadhaa kabla ya hapo. Awali walifanya kazi pamoja katika wimbo wao, I Can’t Get Enough (2019) ambao ulichanganya lugha ya Kiingereza na Kihispania.

“Kwa kweli nina rafiki yangu mkubwa ambaye ninaweza kufanya naye kila kitu duniani, na kila siku huwa ndiyo siku bora zaidi katika maisha yangu,” alisema Blanco hapo Novemba 2024 katika mahojiano na jarida la People.

Akiwa kama mtayarishaji muziki, Blanco amewahi kufanya kazi na wasanii wengi maarufu duniani, miongoni mwa ni Ed Sheeran, Katy Perry, Justin Bieber na The Weeknd.

Kwa mara ya kwanza Selena alitangaza kumchumbiwa na Blanco mnano Desemba 2024, ambapo kupitia Instagram alionyesha pete yake ya uchumba. Katika maelezo ya picha hiyo aliandika, “Milele yetu inaanza sasa...”.

Rafiki wa Selena, mwanamuziki Taylor Swift alikuwa miongoni mwa watu wa kwanza kumpongeza baada ya kutangaza uchumba huo. Taylor Swift, mshindi wa Grammy mara 14, katika post ya Selena aliandika; Vizuri sana, nitakuwa msichana wa kubeba maua kwenye harusi yenu.

Hatimaye Septemba 27, 2025, Blanco na Selena walifunga ndoa katika jimbo la California, Marekani. Mwimbaji huyo alitangaza habari hizo kupitia Instagram. Wakati huo chanzo kimoja kiliuambia mtandao wa People kuwa wawili hao waliandaa sherehe nzuri kwa ajili yao na wageni wao.

“Harusi yao iliwagusa wageni kiasi cha kuwafanya baadhi yao kutoa machozi. Wawili hao waliandika wenyewe viapo vyao vya ndoa. Kila mtu alikuwa na furaha, walisherehekea ndoa yao hadi usiku wa manane. Kulikuwa na vibes kubwa sana,” kilieleza chanzo hicho.

Katika kuhadhimisha mwaka mmoja wa ndoa yao hapo Septemba mwaka huu, Selena alisema kuwa yeye na mume wake bado wanafurahia maisha ya ndoa kama watu walio kwenye kipindi cha fungate.

Ikumbukwe katika tasnia ya burudani, Selena Gomez alianza kupata umaarufu kupitia uigizaji ambapo alianza uigizaji kwenye kipindi cha runinga cha watoto, Barney & Friends mwaka 2002 hadi 2004, kisha kuibukia kipindi cha Disney, Wizards of Waverly Place.