Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Mastaa wataka Maguire apewe dili jipya fasta

MAGUERE Pict

Muktasari:

Beki huyo wa England amepitia kipindi cha misukosuko mingi huko Old Trafford tangu alipojiunga kwa Pauni 85 milioni akitokea Leicester City mwaka 2019.

MANCHESTER, ENGLAND: MASTAA wenzake beki wa kati Harry Maguire wanataka mabosi wa Manchester United kuhakikisha wanampa beki huyo mkataba mpya.

Beki huyo wa England amepitia kipindi cha misukosuko mingi huko Old Trafford tangu alipojiunga kwa Pauni 85 milioni akitokea Leicester City mwaka 2019.

Alinyang’anywa unahodha wa Man United chini ya kocha wa zamani Erik ten Hag, Julai 2023 na akalengwa na kejeli kutoka kwa baadhi ya mashabiki kufuatia mfululizo wa viwango visivyoridhisha.

Hata hivyo, mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 32 ameonekana kuwa wa muhimu katika kikosi katika nyakati za hivi karibuni, hata akitumika kama mshambuliaji wa dharura chini ya kocha mkuu aliyeondolewa, Ruben Amorim.

Hivi karibuni zaidi, ameunda ushirikiano mzuri kwenye safu ya ulinzi sambamba na Lisandro Martinez chini ya kocha wa mpito Michael Carrick, hali iliyomfanya Maguire kutajwa kuwa mchezaji bora wa mechi katika ushindi wa 3-2 wa Man United dhidi ya Arsenal mwezi uliopita.

Mkataba wake wenye thamani ya Pauni 190,000 kwa wiki unamalizika mwishoni mwa msimu huu na klabu kadhaa zimeonyesha nia ya dhati kwa ajili ya kupata saini ya kwa beki huyo mzaliwa wa Sheffield.

Lakini, chumba cha kubadilishia nguo cha Old Trafford kimeungana katika msimamo kwamba viongozi wa klabu wanapaswa kumzawadia mkataba mpya. Chanzo kilisema: “Wachezaji wanaamini itakuwa wazimu kama hatapewa mkataba mpya.

“Harry amepitia mengi mazuri na mabaya akiwa Man United, lakini amevuka yote hayo na kwa sasa anacheza vizuri sana. Anaheshimika sana ndani ya kikosi na anawapa ushauri na uzoefu wachezaji chipukizi kama Ayden Heaven na Leny Yoro. Kila mtu anampenda na kumheshimu na wachezaji wengi wanataka klabu impe mkataba.”

Iwapo Man United itampa ofa mpya, kuna uwezekano mkubwa kuwa itakuwa na mshahara wa chini kidogo ya anaopokea sasa wa kila wiki, lakini ukiwa na bonasi zaidi kulingana na kiwango na mafanikio. Mchezaji huyo wa kimataifa wa England amefunga jumla ya mabao 17 na kutoa asisti tisa katika mechi 261 alizoichezea Man United katika kipindi cha miaka saba.


MAVITU YA MAGUIRE MAN UNITED

-Amecheza: Mechi 13

-Uwanjani: Dakika 772

-Amegonga: Faulo 7

-Amepiga: Pasi 375

-Amefunga: Bao 1