Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Mastaa Man United wataka mabadiliko!

Muktasari:

  • Amorim, 40, ametua Man United na kutambulisha mtindo wake wa uchezaji wa 3-4-3, jambo ambalo linaonekana kuwa ni mtihani mzito kwa mastaa hao wa Old Trafford tangu Novemba mwaka jana.

MANCHESTER, ENGLAND: KUMEKUCHA. Mastaa wa Manchester United wameanza kuhoji mfumo wa kocha wao Ruben Amorim wakimtaka bosi huyo Mreno kubadili staili yake ili mambo yaende sawa, imeelezwa.

Amorim, 40, ametua Man United na kutambulisha mtindo wake wa uchezaji wa 3-4-3, jambo ambalo linaonekana kuwa ni mtihani mzito kwa mastaa hao wa Old Trafford tangu Novemba mwaka jana.

Wachezaji wake wameshindwa kuendana na staili ya uchezaji na kujikuta ikipoteza mara nane katika mechi 20 za michuano yote ambayo Man United imeongozwa na kocha Amorim.

Kiwango kibovu kimefanya Man United ishike nafasi ya 13 kwenye msimamo wa Ligi Kuu England.

Kwa mujibu wa Mail, baadhi ya mastaa wa Man United wamezungumza juu ya uwezekano wa kocha wao kubadili mtindo wake wa kiufundi kuanzia sasa ili timu ipate matokeo ya kuwaweka pazuri.

Kinachoelezwa ni kwamba mambo hayawezi kuwa mazuri kwenye kikosi hicho kama Amorim hatabadilika. Na kinachoonekana, kocha huyo wa zamani wa Sporting CP haonekani kama atabadili mfumo wake wa uchezaji.

Baada ya kichapo cha mabao 2-0 kutoka kwa Newcastle, Desemba mwaka jana, Amorim alisema: "Lazima nitambulishe mtindo wangu. Kama nitabadilika kila wakati mambo yatakuwa mazuri.

"Nafahamu kuna ugumu mkubwa kwa sababu kwa miaka miwili walikuwa wanacheza mtindo tofauti na huu wanaopaswa wacheze kwa sasa. Kupoteza mechi nyingi hilo ni jambo gumu kwao. Unaweza kuona, najaribu kutambulisha mtindo wangu na sina mwingine.

"Unapobadili kocha, hasa kwenye klabu za aina hii, na kwa sababu hawashindi mechi, watapaswa kucheza kwa mfumo ambao utaletwa, ambao unaweza kuwa sahihi."

Licha ya kuwapo na mazungira hayo ya kulalamikia mtindo wa uchezaji, lakini kocha Amorim bado anapewa sapoti kubwa kwenye vyumba vya kubadilishia kwenye kikosi hicho cha Man United.

Beki wa zamani wa Man United, Gary Neville, naye ameibua wasiwasi mkubwa wa kuhusu wachezaji wa timu hiyo wanavyoshindwa kuendana na mtindo ambao kocha Amorim anataka timu hiyo icheze.

Gary Neville alisema: "Nilidhani mambo yatakuwa mazuri baada ya Ruben Amorim kuja, ile morali yake pamoja na mtindo wa uchezaji, wachezaji wanapaswa kuelewa mfumo mpya na kuutumia. Lakini, mambo yamekuwa mabaya zaidi."


Rekodi za makocha wa man united idadi ya mechi walicheza nyumbani kabla ya kupoteza mechi tano.

-Ruben Amorim  - mechi 7

-David Moyes - mechi 14

-Erik ten Hag - mechi 28

-Louis van Gaal - mechi 30

-Ole Gunnar Solskjaer - mechi 31

-Alex Ferguson - mechi 88