PSG yajiondoa dili la Michael Olise
Muktasari:
- Klabu hiyo ya Ufaransa haipo tayari kufikia thamani ya Euro 200 milioni inayotakiwa na Bayern, hali inayompa nafasi kubwa Real Madrid kuendelea na mipango ya kumpeleka Santiago Bernabeu.
Paris Saint-Germain imejiondoa kwenye mbio za kumsajili winga wa Bayern Munich, Michael Olise, baada ya kukataa kushiriki vita ya dau kubwa la uhamisho.
Klabu hiyo ya Ufaransa haipo tayari kufikia thamani ya Euro 200 milioni inayotakiwa na Bayern, hali inayompa nafasi kubwa Real Madrid kuendelea na mipango ya kumpeleka Santiago Bernabeu.
Olise, ambaye amekuwa mmoja wa wachezaji bora Bundesliga, anatajwa kuwa na ndoto ya kujiunga na Real Madrid baada ya msimu bora akiwa Bayern Munich.
Nyota huyo wa kimataifa wa Ufaransa alimaliza msimu akiwa na mabao 22 na pasi za mwisho 31 katika mashindano yote, kiwango kilichovutia vigogo wengi Ulaya.
Rais wa Real Madrid, Florentino Perez, anaamini Olise ana uwezo wa kuwa nyota mkubwa wa kizazi kipya na kuongeza nguvu katika safu ya ushambuliaji inayomuongoza Kylian Mbappe.
Hata hivyo, Bayern Munich haitaki kumuachia kirahisi mchezaji huyo ambaye bado ana mkataba na klabu hiyo.
PSG imeamua kubadilisha mkakati wake wa usajili kwa kuangalia zaidi vipaji vijana badala ya kuingia kwenye vita za gharama kubwa.
Marcus Rashford
Marcus Rashford amezikataa ofa kadhaa kutoka klabu za nje ya England licha ya kipengele chake cha kuondoka Manchester United kwa pauni milioni 40 kumalizika muda wake.
Sasa klabu yoyote itakayomtaka italazimika kufanya mazungumzo ya moja kwa moja na Manchester United kuhusu ada ya uhamisho wake.
Julian Alvarez
Julian Alvarez ameendelea kuhusishwa na Barcelona baada ya kuomba kuondoka Atletico Madrid.
Hata hivyo, viongozi wa Atletico wamesisitiza hawana mpango wa kumuuza mshambuliaji huyo wa Argentina, wakieleza bado ana mkataba wa muda mrefu na ni sehemu muhimu ya mipango ya kocha Diego Simeone.
Maxime Esteve
Maxime Esteve yupo mbioni kujiunga na RB Leipzig kutoka Burnley kwa ada inayokadiriwa kufikia pauni milioni 27.3.
Burnley imekubali kumuuza beki huyo baada ya kushuka daraja, huku Leipzig ikiamini uwezo wake utaongeza uimara wa safu ya ulinzi katika msimu ujao wa Bundesliga.
Djed Spence
Djed Spence ameibuka kuwa lengo kuu la Inter Milan baada ya kiwango kizuri alichoonyesha katika Kombe la Dunia.
Klabu hiyo ipo tayari kuongeza ofa yake, huku Tottenham ikitajwa kutaka kati ya pauni milioni 30 na 35 ili kumruhusu beki huyo kuondoka.
Jhon Duran
Jhon Duran anakaribia kujiunga na Benfica kwa mkopo kutoka Al-Nassr baada ya kushindwa kung’ara Saudi Arabia.
Klabu ya Benfica inaamini mshambuliaji huyo wa Colombia atarejea katika kiwango chake, huku Al-Nassr ikikubali kugharamia sehemu kubwa ya mshahara wake msimu ujao.
Kayne van Oevelen
Kayne van Oevelen anaendelea kuwindwa na Ipswich Town baada ya ofa ya kwanza kukataliwa na FC Volendam.
Klabu hiyo ya England inajiandaa kuongeza dau lake, huku Valencia pia ikifuatilia kwa karibu maendeleo ya mazungumzo ya kumsajili kipa huyo wa Uholanzi.
Lucas Bergvall
Lucas Bergvall ameibuka kuwa lengo kuu la Nottingham Forest baada ya kuondoka kwa Elliot Anderson kuelekea Manchester City, lakini Tottenham imekataa ofa ya kwanza kwa kiungo huyo wa Sweden. Forest inatarajiwa kurejea na dau jipya, huku Spurs wakisisitiza kuwa watamuuza endapo thamani wanayoitaka itafikiwa.
Romelu Lukaku
Romelu Lukaku anaweza kuondoka Napoli dirisha hili la usajili huku klabu hiyo ikitaka kupunguza matumizi ya mishahara.
Ajax, Monaco na Fenerbahce zinaendelea kumfuatilia, lakini New York City FC ya Marekani nayo imeingia kwenye mbio za kumsajili mshambuliaji huyo wa kimataifa wa Ubelgiji.
Karim Adeyemi
Karim Adeyemi yupo hatua za mwisho kujiunga na Barcelona baada ya kukamilisha vipimo vya afya kwa makubaliano ya uhamisho kutoka Borussia Dortmund.
Dili hilo lenye thamani ya Euro 29 milioni, kabla ya mshambuliaji huyo wa Ujerumani kutambulishwa rasmi na kuanza mazoezi chini ya Kocha Hansi Flick msimu ujao.