Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Mashabiki Man United wakinukisha

KIMENUKA Pict

Muktasari:

  • Man United bado haijashinda mchezo wowote kwenye Ligi Kuu England msimu huu baada ya kubanwa na Fulham na kufungana 1-1,  Jumapili uwanjani Craven Cottage. Mechi ya kwanza, miamba hiyo ya Old Trafford ilikubali kipigo cha bao 1-0 kutoka kwa Arsenal.

MANCHESTER, ENGLAND: KIMENUKA. Ndicho unachoweza kusema baada ya mashabiki wa Manchester United kuripotiwa kutoa maoni ya kutaka kocha Ruben Amorim afutwe kazi kwa kitendo chake cha kumfanya kiungo Kobbie Mainoo kuwa chaguo la nne kwenye kikosi hicho cha Old Trafford.

Man United bado haijashinda mchezo wowote kwenye Ligi Kuu England msimu huu baada ya kubanwa na Fulham na kufungana 1-1,  Jumapili uwanjani Craven Cottage. Mechi ya kwanza, miamba hiyo ya Old Trafford ilikubali kipigo cha bao 1-0 kutoka kwa Arsenal.

Man United ilishinda mechi nane zilizopita uwanjani Craven Cottage, lakini kwa Jumapili ilishindwa kuendeleza ubabe huo. Kikosi hicho cha Kocha Amorim, kwenye mechi dhidi ya Fulham kilitangulia kwa bao la kujifunga la Rodrigo Muniz, lakini Emile Smith Rowe alisawazisha baada ya kutokea benchini.

Baada ya kushuhudia kikosi chake kikipata shida eneo la kiungo, Amorim aliamua kuanza na pacha ya kiungo Bruno Fernandes na Casemiro, ambaye baadaye alimtoa na kumuingiza Manuel Ugarte. Hata hivyo, staa wa kimataifa wa England, Mainoo aliendelea kubaki benchi na kocha Amorim alichagua kutomtumia kabisa katika mechi hiyo. Na hilo limewakasirisha mashabiki wa Man United na kumtaka kocha huyo aanze kumtumia kiungo huyo. Na kuna baadhi ya wamefikia hatua ya kutaka Amorim aondoke baada ya kutumia Pauni 200 milioni kwenye kusajili washambuliaji wapya na bado Man United imeshindwa kufunga bao kupitia mchezaji wake katika mechi mbili za ligi ilizocheza.

Shabiki mmoja alisema: “Kobbie Mainoo anachukuliwa kama chaguo la nne la safu ya kiungo, hili linashtua.”

Mwingine alisema: “Hebu fukuza huyo Amorim, alikuwa na mwaka wa kuonyesha kitu na hakuna alichofanya. Hakuna maendeleo, hakuna maboresho, hakuna mipango. Hakuna kinachofanya aendelee kubaki.”

Kuna shabiki alisema: “Amorim anaonekana kumjaribu kila mtu kwenye sehemu ya kiungo ya kati isipokuwa Mainoo, hii kitu inakwaza.”

Shabiki wa nne alisema: “Bruno, kucheza dakika nyingine 90 bila ya kufanyiwa mabadiliko. Yeye kuwa asiyewekwa benchi itasababisha Amorim kufutwa kazi.”

Shabiki wa tano alisema: “Hii kitu ya Amorim kushindwa kucheza 4-3-3 na kumpa nafasi Mainoo kwenye timu itamfanya afukuzwe kazi.”

Shabiki mwingine aliongeza: “Siwezi kumtetea kocha ambaye anamtoa Amad na kumwingiza Dalot, anamchezesha Mount kwenye kiungo ya kukaba badala ya Mainoo, anamwingiza Ugarte kwenye kila mechi na bado anafanya ovyo uwanjani, mtu anayeingiza mabeki wawili wakati anataka ushindi na kuwaacha Mainoo  na Zirkzee kwenye benchi.”

Katika mechi hiyo ya Fulham, Man United nafasi pekee ya wazi ya kufunga ilitengenezwa na mchezaji asiyetabirika kabisa. Na nafasi hiyo ni ile pasi ndefu ya kipa Altay Bayindir kwa mchezaji Matheus Cunha, ambaye shuti lake lilipanguliwa na kipa Bernd Leno na mpira kutoka nje.

Hilo liliwaibua mashabiki na kutoa maoni yao kwenye mtandao wa X, ambapo mmoja alisema: “Kipa anapokuwa mchezeshaji, hiyo inaweza kuona hali ilivyo.”

Shabiki mwingine alisema: “Baada ya kutumia zaidi ya Pauni 200 milioni kwa washambuliaji bado unahitaji kipa anatengeneza nafasi ya kufunga.”