Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Manchester City yamsaka mrithi wa Rodri

MRITHI Pict

Muktasari:

  • Kocha Enzo Maresca amesema City italazimika kutafuta “Rodri mpya” baada ya kiungo huyo mwenye umri wa miaka 30 kuondoka Etihad na kusaini mkataba wa miaka minne Barcelona.

MANCHESTER, ENGLAND: MANCHESTER City imeanza mchakato wa kutafuta mrithi wa kiungo Rodri baada ya nahodha huyo wa Hispania kuondoka klabuni hapo na kujiunga na mabingwa wa La Liga, Barcelona.

Kocha Enzo Maresca amesema City italazimika kutafuta “Rodri mpya” baada ya kiungo huyo mwenye umri wa miaka 30 kuondoka Etihad na kusaini mkataba wa miaka minne Barcelona.

Barcelona imekubali kulipa ada inayokadiriwa kufikia pauni65 milioni kwa ajili ya kumsajili Rodri, ambaye alitumia misimu saba akiwa City na kuwa miongoni mwa viungo bora duniani.

Akiwa City, Rodri alishinda tuzo ya Ballon d’Or mwaka 2024, mataji manne ya Ligi Kuu England pamoja na Ligi ya Mabingwa Ulaya, akifunga bao pekee katika fainali ya mwaka 2023 dhidi ya Inter Milan.

Kiungo huyo pia aliisaidia Hispania kutwaa Kombe la Dunia msimu huu kabla ya kuhamia Barcelona.

MRI 04

Akizungumza kuhusu namna City itakavyoshughulikia pengo lake, Maresca amesema“tutatatua vipi tatizo hilo? Tutajaribu kumpata Rodri mpya, ndivyo ilivyo.

“Kabla Rodri hajaja hapa, hakuwa ameshinda Ballon d’Or, hakuwa ameshinda Ligi ya Mabingwa wala Kombe la Dunia la Klabu. Alijiunga na klabu hii, kisha akafanikiwa kupata mafanikio mengi muhimu.”

MRI 01

Rodri aliichezea City karibu michezo 300 kabla ya kuondoka akiwa katika miezi 12 ya mwisho ya mkataba wake.

Ingawa City ilikuwa imempa ofa ya kuongeza mkataba, mazungumzo hayakuzaa matunda na hatimaye Barcelona ikafanikiwa kumpata.

Maresca amesema kuondoka kwa wachezaji wakubwa si jambo geni katika historia ya City, akitolea mfano wa David Silva, Kevin De Bruyne, Sergio Aguero na Fernandinho.

MRI 02

“Nilikuwa nikifikiria Alhamisi usiku, wakati David Silva alipokuwa hapa, kila mtu alikuwa na wasiwasi, kisha Kevin [De Bruyne] akaja.

“Sergio [Aguero] alipokuwa hapa, kila mtu alikuwa na wasiwasi kuhusu siku atakapoondoka, kisha Erling [Haaland] akaja. Fernandinho aliondoka, Rodri akaja.”

Kwa mujibu wa Maresca, jambo muhimu kwa City ni kuwa na ufanisi katika usajili kila inapompoteza mchezaji muhimu.

MRI 03

“Wakati wanaondoka, unahitaji kuwa mzuri katika kumsajili anayefuata. Wote hao ni sehemu ya mabadiliko. David, Kevin, Fernandinho, Rodri, Erling, kuna mwingine pia.

“Ni kawaida, ni mabadiliko. Sio tatizo. Unaendelea na kujaribu kufanya mambo sahihi.”

City sasa ina kazi ya kutafuta kiungo atakayeweza kuziba pengo kubwa lililoachwa na Rodri, ambaye amekuwa mhimili wa mafanikio ya klabu hiyo katika miaka ya karibuni.