Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Man Utd mpo? Haaland ana meseji yenu huko!

HAALAND Pict

Muktasari:

Norway inakaribia kufuzu fainali zake za kwanza za Kombe la Dunia tangu 1998 na straika wao wa mabao, Haaland amehakikisha jambo hilo linawezekana baada ya kufunga mabao matano kwenye mechi moja siku chache tu kabla ya kwenda kujiunga na chama lake la Manchester City litakalokuwa uwanjani Etihad kukipiga na mahasimu wao Man United kwenye mechi ya lazima ushindi kwa timu zote mbili.

MANCHESTER, ENGLAND: STRAIKA Erling Haaland atuma ujumbe mzito kwa Manchester United kwa ajili ya kipute cha Manchester derby Jumapili baada ya kufunga mabao matano wakati Norway ilipoangusha kipigo kizito kwa Moldova kwa kushinda 11-1 kwenye kufuzu fainali za Kombe la Dunia 2026.

Norway inakaribia kufuzu fainali zake za kwanza za Kombe la Dunia tangu 1998 na straika wao wa mabao, Haaland amehakikisha jambo hilo linawezekana baada ya kufunga mabao matano kwenye mechi moja siku chache tu kabla ya kwenda kujiunga na chama lake la Manchester City litakalokuwa uwanjani Etihad kukipiga na mahasimu wao Man United kwenye mechi ya lazima ushindi kwa timu zote mbili.

Haaland tayari ameshafunga mabao matatu kwenye mechi tatu alizocheza kwenye Ligi Kuu England msimu huu, lakini kikosi chake cha Man City kikiambulia pointi tatu tu baada ya kushinda moja na kuchapwa mbili kwenye mechi hizo. Man City inahitaji ushindi wa lazima dhidi ya mahasimu wao hao na Haaland anaonekana kuwa kwenye wakati wake.

Straika Haaland alifunga mabao matatu ndani ya dakika 32 za kipindi cha kwanza katika kipute hicho kilichopigwa uwanjani Ullevaal, mjini Oslo ambapo ilikuwa hat-trick yake ya tano kwenye kikosi cha timu ya taifa. Aliongeza mabao mawili kwenye kipindi cha pili na kuasisti mara mbili.

Kiungo wa Rangers, Thelo Aasgaard alitokea benchini na kufunga mabao manne kwenye kipindi cha pili. Na sasa, Haaland amefunga mabao tisa kwenye mechi za kufuzu Kombe la Dunia, ikiwa ni idadi kubwa ya mabao ukilinganisha na wachezaji wengine, huku ubora wake umekuja kipindi hiki cha kuelekea kwenye mchezo wa kuwakabili Man United uwanjani Etihad.

Haaland, 25, amekuwa mchezaji wa kwanza kufunga mabao matano kweye mechi moja kwa timu yake ya Norway tangu mwaka 1948 na alisema: “Ni mechi ngumu, tumepambana kuanzia mwanzo hadi mwisho. Imekuwa jioni ya kihistoria!”

Staa wa Arsenal, Odegaard alisema ilikuwa ndoto kucheza na Haaland na kumwagia sifa zake straika huyo wa Man City, aliposema: “Ni ndoto kucheza naye. Nafahamu namna anavyokuwa na mikimbio mizuri uwanjani. Na linapokuja suala la kupiga mashuti, yeye atakumaliza.”

Na mchezaji mwenzao kwenye timu ya taifa, anayechezea Fulham, Sander Berge alisema yeye alichokuwa akifanya ni kuketi tu na kuwaangalia wawili hao, Haaland na Odegaard wakifanya mambo yao uwanjani.