Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Man United v Newcastle… hii mechi imeshtua!

Muktasari:

  • Mabingwa watetezi wa Ligi Kuu England, Liverpool walinyakua pointi zote tatu katika mechi hiyo ya ugenini, shukrani kwa bao la dakika za majeruhi lililofungwa kwenye dakika ya 100 ya mchezo na kinda Rio Ngumoha.

LONDON, ENGLAND: NI kasheshe, unaweza kusema hivyo. Hii ni baada ya aliyekuwa mkuu wa waamuzi wa kulipwa kwenye Ligi Kuu England, Keith Hackett, kusema mechi ya Liverpool ya ushindi wa 3-2 dhidi ya Newcastle United inapaswa kuchunguza.

Mabingwa watetezi wa Ligi Kuu England, Liverpool walinyakua pointi zote tatu katika mechi hiyo ya ugenini, shukrani kwa bao la dakika za majeruhi lililofungwa kwenye dakika ya 100 ya mchezo na kinda Rio Ngumoha.

Liverpool ilionekana kuwa kwenye wakati mzuri wa kushinda baada ya kuwa mbele kwa mabao 2-0, yaliyofungwa na Ryan Gravenberch na Hugo Ekitike, huku wenyeji wa mchezo, Newcastle United wakibaki 10 uwanjani kufuatia Anthony Gordon kutolewa kwa kadi nyekundu kwa kumchezea rafu Virgil van Dijk kwenye kipindi cha kwanza.

Lakini, Newcastle iliyocheza bila ya huduma ya straika wao Alexander Isak, ilipambana na kusawazisha mabao hayo, kupitia kwa Bruno Guimaraes na mtokea benchini Will Osula kufanya ubao wa matokeo usomeke 2-2. Jambo hilo liliitisha Liverpool hadi hapo kinda Ngumoha alipofunga la ushindi kwenye dakika za majeruhi.

Hata hivyo, mechi hiyo imekosolewa sana kutokana na namna ilivyokuwa ikisimamasimama mara nyingi na jinsi mpira ulivyokuwa mchezoni kwa muda mdogo.

Kulikuwa na faulo 32 katika mechi hiyo, huku Newcastle ikipoteza pia wachezaji wake watatu kutokana na kuumia, ambao walisimamisha mchezo pia.

Kwa mujibu wa takwimu za Opta, mpira ulikuwa mchezoni kwa asilimia 40.8 tu ya mchezo wote. Kwa maana hiyo, asilimia 59.2 mpira ulikuwa umesimama haukuwa mchezoni na hivyo ikidaiwa ni hasara kubwa kwa mashabiki.

Hiyo ni idadi ndogo sana ya muda kwenye mechi za Ligi Kuu England kwa miaka 15, tangu Stoke City ilipoichapa Blackburn Rovers, Februari 2010.

Bosi wa zamani wa waamuzi, Hackett alisema namba hizo hazikubaliki na kuitaka Ligi Kuu England kufanya uchunguzi, licha ya kwamba amemtetea refa wa mchezo huo wa St James’ Park, Simon Hooper.

Akizungumza na Football Insider, Hackett alisema: “Kusema ukweli hii haikubaliki, inashindwa kutoa uhalisia wa thamani ya pesa ambayo mashabiki wanalipa. Napendekeza Ligi Kuu England ifanye uchunguzi kujua ni eneo gani muda ulipotea zaidi.

“Hooper ni mwamuzi anayependa kuweka mambo sawa ili mechi iendee vizuri. Naweza kusema hapaswi kulaumiwa, lakini ni dhahiri anaweza kuwa na umuhimu mkubwa wa kutunza muda hasa kutokana na dakika alizoongeza.

“Mechi ilikuwa na matatizo, ambayo huwezi kuyafumbia machi, Ligi Kuu England lazima ifanye uchunguzi.”