Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Man United yamnasa kiungo Ubelgiji

MAN UTD Pict

Muktasari:

  • United imeweka kipaumbele kusajili viungo dirisha hili la usajili, lakini imekumbana na vikwazo baada ya kushindwa kuwapata malengo yake ya awali.

LONDON, ENGLAND: Manchester United ipo katika hatua za mwisho za mazungumzo ya kumsajili kiungo wa Aston Villa, Youri Tielemans, katika harakati za kuimarisha safu yao ya kiungo kabla ya msimu mpya.

United imeweka kipaumbele kusajili viungo dirisha hili la usajili, lakini imekumbana na vikwazo baada ya kushindwa kuwapata malengo yake ya awali.

Kiungo Elliot Anderson ameichagua Manchester City, huku Mateus Fernandes akiamua kujiunga na Tottenham Hotspur badala ya kwenda Old Trafford.

Awali, United ilikuwa imefikia makubaliano ya pauni milioni 35 na Atalanta kwa ajili ya kumsajili kiungo wa Brazil, Ederson, lakini dili hilo limesimamishwa kwa sasa.

Wakati huohuo, Andrey Santos wa Chelsea anaripotiwa tayari kufanyiwa vipimo vya afya kabla ya kukamilisha uhamisho wa pauni milioni 48 kwenda United, huku klabu hiyo ikiendelea kutafuta nyongeza zaidi kikosini.

Kwa sasa, kiungo pekee mwenye uzoefu mkubwa katika nafasi ya kiungo wa kati ndani ya United ni Kobbie Mainoo, ambaye bado hajapata nafasi ya kucheza na England katika Kombe la Dunia 2026.

Taarifa zinaeleza kuwa mkataba wa Tielemans na Aston Villa una kipengele kinachoruhusu kuondoka endapo dau lililowekwa litalipwa, jambo ambalo limeifanya United kuwa karibu zaidi kukamilisha usajili huo.

Kiungo huyo mwenye umri wa miaka 29 amekuwa akifuatiliwa na United kwa muda mrefu kutokana na uzoefu wake mkubwa wa Ligi Kuu England, jambo ambalo viongozi wa klabu hiyo wanaamini litakuwa msaada mkubwa kwa kikosi.

Tielemans alikuwa mmoja wa wachezaji muhimu wa Ubelgiji katika safari yao ya kutinga robo fainali ya Kombe la Dunia 2026, lakini alikosa mchezo wa robo fainali dhidi ya Hispania uliomalizika kwa kipigo cha mabao 2-1 baada ya kupata majeraha wakati wa maandalizi ya mwisho kabla ya mechi.