Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Man City yapigwa tena, West Ham safi

CITY Pict

MANCHESTER, ENGLAND: Manchester City imeendelea kuwa na matokeo mabaya kwenye Ligi Kuu England, Premier League baada ya kulala kwa mabao 2-1 dhidi ya Brighton.

City imepoteza michezo miwili kati ya mitatu ambayo imecheza hivi karibuni na sasa kuna presha kubwa kuwa kocha wa timu hiyo, Pep Guardiola anaweza kutimuliwa.

Katika mchezo huu, City ilikuwa ya kwanza kupata bao kupitia kwa Erling Haaland katika dakika ya 34 ya mchezo huo.

Hata hivyo, kipindi cha pili kilikuwa kichungu kwao baada ya Brighton kubadilika na kuutawala mchezo huo, ambapo ilifanikiwa kujipatia mabao kupitia kwa James Milner aliyefunga kwa mkwaju wa penalti dakika ya 67.

Wakati mashabiki wakiamini kuwa mchezo huo utamalizika kwa sare, Brajan Gruda aliwafanya kitu kibaya mabeki wa City na kufunga bao safi katika dakika ya 88 ya mchezo huo na kuipa timu yake ushindi huo muhimu.

Katika michezo mitatu ya ligi hiyo, City ilipoteza mchezo dhidi ya Spurs kwa kulala mabao 2-0, lakini ikafanikiwa kupata ushindi wa mabao 4-0 dhidi ya Wolves.

Sasa michezo mitatu ya timu hiyo inayofuata itavaana na Man United, Napoli kwenye Ligi ya Mabingwa Ulaya, halafu Arsenal. 
Mchezo mwingine umewashuhudia West Ham wakiibuka na ushindi wa mabao 3-0 dhidi ya Nottigham Forest.

Mabao ya West Ham yamefungwa na Jarrod Bowen, Lucas Paquenta na Calum Wilison.