Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Mambo yalivyokuwa moto Italia, Hispania, Ujerumani

MAMBO Pict

Muktasari:

  • Mshambuliaji Ferran Torres aliingia uwanjani akitokea benchi na kufunga mabao mawili ya kusawazisha mwishoni mwa mchezo katika mechi yake ya kwanza, huku PSG ikitoka nyuma kwa mabao mawili na kulazimisha sare ya 2-2 dhidi ya wenyeji Rennes, Jumapili.

PARIS, UFARANSA: MAMBO yameanza kuwa moto. Ligi kuu tano za soka Ulaya zilirejea zote wikiendi iliyopita. Achana na Iile ya England iliyoanzisha msimu wa 2026/27 Ijumaa kwa mechi kati ya Arsenal na Coventry City ambao mabingwa watetezi walishinda kwa maba 3-0, kule Ufaransa, Ligue 1 ilirudi na makali yake.

Mshambuliaji Ferran Torres aliingia uwanjani akitokea benchi na kufunga mabao mawili ya kusawazisha mwishoni mwa mchezo katika mechi yake ya kwanza, huku PSG ikitoka nyuma kwa mabao mawili na kulazimisha sare ya 2-2 dhidi ya wenyeji Rennes, Jumapili.

Sebastian Szymanski na Esteban Lepaul waliipa Rennes uongozi wa mabao 2-0 hadi mapumziko, lakini PSG iliongeza presha kipindi cha pili na hatimaye kupata pointi moja. Rennes ilifunga ndani ya dakika tisa za kwanza, baada ya shuti la Szymanski kugonga mwamba wa lango na kuingia, ukiwa mwanzo mzuri wa msimu kwa wenyeji.

Desire Doue alidhani amesawazisha kwa PSG, lakini bao lake lilikataliwa kwa sababu ya kuotea. Rennes ikaongeza bao la pili dakika saba kabla ya mapumziko. Przemyslaw Frankowski alipata nafasi upande wa kulia na krosi yake ya chini ndani ya eneo la hatari ikageuzwa na Lepaul na kuingia wavuni.

PSG ilipunguza pengo dakika 19 kabla ya mchezo kumalizika, baada ya Torres kufanya mikimbio mizuri kuvuka mtego wa kuotea, akapokea pasi ya Fabian Ruiz na kufunga bao lake la kwanza kwa klabu hiyo tangu alipojiunga akitokea Barcelona msimu huu.

Torres alisawazisha dakika ya 83, huku Ruiz akiwa tena mtoa pasi, safari hii akitoa kutokea upande wa kushoto. Wachezaji hao wawili kutoka Hispania waliirudisha PSG kwenye mchezo, lakini hawakuweza kuisaidia timu yao kupata bao la ushindi.

MAMB 04

Atletico yachomoa

Atletico Madrid ililazimisha sare ya 2-2 dhidi ya Villarreal katika Ligi Kuu Hispania (La Liga), licha ya kumaliza mchezo ikiwa beki Robin Le Normand akionyeshwa kadi nyekundu.

Winga Giuliano Simeone aliisawazishia Atletico baada ya Villarreal kuongoza kufuatia mabao ya penalti yaliyofungwa na Gerard Moreno na Georges Mikautadze, baada ya Marc Pubill kuifungia Villarreal bao la kwanza dakika ya 59.

Kocha wa Atletico Madrid, Diego Simeone, alimwingiza Julian Ãlvarez kipindi cha pili, lakini mashabiki nyumbani walimzomea. Mshambuliaji huyo alilazimika kutoka akiwa peke yake kwenye vyumba vya kubadilishia nguo baada ya mchezo, wakati wachezaji wenzake wakiwash ukuru mashabiki wa Atletico.

MAMB 01

Amorim atoboa na Milan yake

Katika Ligi Kuu Italia (Serie A), kulikuwa na mechi nyingi, lakini iliyotazwa zaidi ilikuwa ni ile ya kwanza kwa Ruben Amorim aliyekuwa katika benchi la ufundi kama kocha wa AC Milan wakiondoka na  ushindi wa mabao 2-1 dhidi ya Torino.

Mchezaji aliyeingia kipindi cha pili, Adrien Rabiot, alitoa asisti kwa Alphadjo Cisse kufunga bao la kwanza dakika ya 64, kabla ya Rabiot mwenyewe kufunga la pili dakika tatu baadaye. Che Adams aliifungia Torino bao la kufutia machozi katika muda wa nyongeza.

Nayo Juventus iliyokuwa ikiangaliwa zaidi kutokana na usajili mpya wa nguvu ilioufanya dirisha hili ilipata ushindi wa ugenini wa bao 1-0 dhidi ya Frosinone, timu iliyopanda daraja msimu huu, lakini haikuonyesha kiwango cha kuridhisha katika mchezo wake wa kwanza wa msimu.

Juve, iliyomaliza nafasi ya sita msimu uliopita ilipata pointi zote tatu kutokana na bao la kichwa la Gleison Bremer dakika ya 22.

Timu hiyo chini ya kocha Luciano Spalletti iliendelea kutawala mchezo, lakini ilishindwa kuongeza bao la pili ili kujiweka katika hali salama.

Kipa Guglielmo Vicario, aliyepo kwa mkopo kutokea Tottenham Hotspur, alipata jeraha la mguu na kulazimika kutolewa mwishoni mwa mchezo. Hali hiyo nusura iigharimu Juventus baada ya Frosinone kuongeza mashambulizi katika muda wa nyongeza na hata kugongesha mwamba wa lango.

Mechi nyingine iliyokuwa ikiangaliwa kwa karibu na wadau wa soka la UIaya kutokana na kumhusisha bingwa na timu kinga’nganizi miongoni mwa zilizopanda daraja, Monza, ilifungwa mabao 4-1 na mabingwa Inter Milan katika mchezo wa ufunguzi wa msimu.

Lecce nayo ilianza msimu kwa ushindi mzuri dhidi ya timu nyingine iliyopanda daraja, Venezia, ambapo Lecce iliwafunga wenyeji 2-0 kupitia mabao ya kipindi cha pili yaliyofungwa na Olaf Gorter na Tiago Gabriel.

MAMB 02

Tuzo ya Kane, Dortmund chali

Kule katika Ligi Kuu ya Ujerumani (Bundesliga), mshambuliaji wa Bayern Munich, Harry Kane, alichaguliwa kuwa Mchezaji Bora wa Mwaka 2026 nchini Ujerumani na Chama cha Waandishi wa Habari za Michezo, Jumapili.

Kane alimaliza mbele ya mwenzake wa Bayern Munich, Michael Olise, ambapo Jarida la Kicker lilitangaza matokeo ya kura ya kila mwaka iliyopigwa na wanachama wa Chama cha Waandishi wa Habari za Michezo cha Ujerumani.

Nahodha huyo wa England alishinda tuzo hiyo baada ya msimu bora ambao Bayern Munich ilitwaa ubingwa wa Bundesliga na Kombe la Ujerumani, huku pia ikifika hatua ya nusu fainali ya Ligi ya Mabingwa Ulaya.

Kocha wa Bayern, Vincent Kompany, alichaguliwa kuwa Kocha Bora wa Mwaka, wakati nahodha wa timu ya wanawake ya Bayern, Giulia Gwinn, akitwaa tuzo ya Mchezaji Bora wa Kike.

Hayo yote yalisindikizwa na kiwango cha Kane ambaye alikuwa mfungaji bora katika msimu uliopita, na pia juzi Bayern ikibeba ubingwa wa michuano ya Ngao ya Jamii Ujerumani maarufu kama DFL-Supercup.

Mabao ya mchezo huo kwa Bayern Munich yalifungwa na Nathaniel Brown dakika ya 28 na Michael Olise ile ya 45+1, huku Borussia Dortmund bao lao likifungwa na Fabio Silva katika dakika ya 75.

MAMB 03

Salah aanza na mawili uturuki

Nje ya ligi tano bora Ulaya, nyota wa kimataifa wa Misri, Mohamed Salah alifunga mabao yake ya kwanza akiwa na Trabzonspor, akitupia mara mbili katika ushindi wa 2-1 dhidi ya Istanbul Basaksehir.

Mshambuliaji huyo wa zamani wa Liverpool alijiunga na timu hiyo ya Super Lig ya Uturuki kwa mkataba wa miaka miwili mwanzoni mwa Agosti.