Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

MAJANGA! Raya kuzikosa Dortmund, Man City, Spur na Real Madrid

MAJANGA Pict

Muktasari:

  • Kipa huyo mwenye umri wa miaka 31 alilazimika kutoka uwanjani dakika ya 70 katika mchezo wa Jumamosi dhidi ya Newcastle United uliomalizika kwa sare ya mabao 2-2, baada ya kuonekana akiumia bega katika tukio la kawaida la kugombea mpira na mshambuliaji wa Newcastle, William Osula.

LONDON, ENGLAND: ARSENAL imepata pigo baada ya kipa wake namba moja, David Raya, kupata majeraha katika kipindi hiki muhimu cha msimu, hali inayoweza kuathiri mipango ya kocha Mikel Arteta kutokana na umuhimu wa kipa huyo katika kikosi cha The Gunners.

Kipa huyo mwenye umri wa miaka 31 alilazimika kutoka uwanjani dakika ya 70 katika mchezo wa Jumamosi dhidi ya Newcastle United uliomalizika kwa sare ya mabao 2-2, baada ya kuonekana akiumia bega katika tukio la kawaida la kugombea mpira na mshambuliaji wa Newcastle, William Osula.

Arsenal inaonekana kuwa na kikosi chenye wachezaji wengi wenye uwezo wa kucheza katika nafasi mbalimbali, kutokana na uwekezaji uliofanywa kukiongezea nguvu kikosi hicho. Hata hivyo, hali ni tofauti katika nafasi ya kipa, ambako chaguo la mbadala linaonekana kuwa na upungufu wa ubora.

Raya alikuwa mhimili muhimu katika kampeni ya Arsenal ya kutwaa ubingwa wa Ligi Kuu England msimu uliopita. Pia alichaguliwa katika kikosi bora cha dunia cha FIFPRO (Men's World 11), huku akikosa kwa bahati mbaya tuzo ya Yashin inayotolewa kwa kipa bora duniani, iliyokwenda kwa mwenzake wa timu ya taifa ya Hispania, Unai Simon.

MAJA 01

Chaguo la kwanza la kumrithi Raya ni Kepa Arrizabalaga, ambaye bado anashikilia rekodi ya kuwa kipa ghali zaidi kuwahi kusajiliwa katika historia ya soka baada ya Chelsea kumsajili kutoka Athletic Bilbao kwa Pauni 72 milioni, Agosti 2018.

Hata hivyo, kwa upande wa ubora, Kepa yuko nyuma ya Raya, ambaye uwezo wake wa kupiga pasi ndefu na kucheza akiwa na mpira miguuni ni sehemu muhimu ya mfumo wa Arsenal katika kuanzisha mashambulizi.

Uwepo wa Raya pia ni miongoni mwa sababu zinazoifanya Arsenal kuwa na safu bora ya ulinzi katika Ligi Kuu England. Hadi sasa, timu hiyo imeruhusu mabao saba pekee katika ligi, idadi inayolingana na Brighton, ambayo imecheza mechi moja pungufu.

MAJA 02

Mbali na Kepa, Arsenal ilisajili pia kipa wa zamani wa Leeds United, Illan Meslier, kwa uhamisho huru katika dirisha la usajili la majira ya kiangazi. Hata hivyo, mchezo wake pekee msimu huu ulikuwa dhidi ya Fleetwood Town ya Ligi Daraja la Nne England, ambapo Arsenal ilipata kipigo cha aibu katika Kombe la Carabao.

Akizungumzia majeraha ya Raya, Arteta amesema bado hajafahamu ukubwa wa tatizo hilo, akieleza kuwa kipa huyo atafanyiwa vipimo zaidi ili kubaini hali yake.

"Kwa bahati mbaya, alilazimika kutoka uwanjani, jambo ambalo si habari njema. Atafanyiwa uchunguzi na kupimwa kwa kutumia mashine ya MRI ili kubaini hasa kilichotokea," amesema Arteta.

"Kwa sasa sijui ilitokeaje wala aina ya jeraha alilopata. Itabidi tusubiri hadi kesho ili kupata majibu."


MAJA 04

RAYA NI NGUZO ISIYOKUWA NA MBADALA

Jeraha la Raya limekuja wakati Arsenal ikijiandaa kuingia katika kipindi kigumu cha ratiba ya michezo, ambacho ndani ya wiki nne itakutana na Borussia Dortmund, Manchester City, Brentford, Tottenham Hotspur na Real Madrid.

Akizungumzia umuhimu wa kipa huyo, mshambuliaji wa zamani wa England, Alan Shearer, ambaye ni mchambuzi wa kipindi cha Match of the Day cha BBC, amesema Raya ni mchezaji ambaye Arsenal haiwezi kumudu kumpoteza.

"Mchezaji mmoja ambaye Arsenal haiwezi kumudu kumpoteza ni David Raya. Ameleta mabadiliko makubwa tangu alipojiunga na klabu hiyo akitokea Brentford mwaka 2023.

"Arsenal ina wachezaji wa kiwango cha juu wanaoweza kuziba nafasi katika maeneo mengine karibu yote, lakini Raya ndiye ambaye Arteta hatapenda kukosa huduma yake kwa kipindi kirefu.

"Kwa kweli, wanaweza kuingia sokoni kusaka kipa mwingine katika dirisha la Januari iwapo watahitaji kufanya hivyo, lakini Arteta atakuwa akitumaini kwa dhati kuwa Raya hatakaa nje kwa muda mrefu," amesema Shearer.

MAJA 03

Umuhimu wa Raya ndani ya kikosi cha Arsenal pia unaonekana katika hatua za klabu hiyo za kutaka kumuongezea mkataba mpya, huku taarifa zikieleza kuwa mazungumzo ya kufikia makubaliano yako katika hatua za mwisho, licha ya kuwa bado ana miaka miwili katika mkataba wake wa sasa.

Naye kiungo wa zamani wa England, Jamie Redknapp, akizungumza kupitia Sky Sports, alieleza kuwa Raya ni kipa asiye na mbadala wa kiwango chake katika kikosi cha Arsenal.

"Kepa hayuko katika kiwango chake. Kwa kweli, naamini anapata wakati mgumu katika Ligi Kuu England. Sote tuliona hali yake katika fainali ya Kombe la Carabao mwaka jana.

"Sasa atalazimika kucheza baadhi ya mechi, jambo ambalo halitakuwa rahisi kwake.

"Hali hii itabadilisha mambo mengi kwa Arsenal kwa kipindi fulani. Hilo ni pigo kubwa, kutegemea Raya atakaa nje kwa muda gani, kwa sababu hawezi kuzibika pengo lake. Pengine ndiye kipa bora zaidi katika Ligi Kuu England, au angalau mmoja wa makipa bora duniani," amesema Redknapp.