Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Conceicao aota kuwa kama Veron

Muktasari:

  • Conceicao, 16, alisema Veron ndiye aliyemvutia zaidi wakati akifuatilia Kombe la Dunia la U-17 mwaka 2019. Wakati huo Veron alikuwa akiichezea Palmeiras, klabu ambayo Conceição pia anaitumikia katika akademi hiyo.

KIUNGO wa Brazil, Eduardo Conceicao amesema anataka kuyatumia mashindano ya Kombe la Dunia U-17 yanayoendelea Qatar ili kufuata nyayo za Gabriel Veron ambaye awali alikuwa akimtazama uwanjani kama shabiki yake.

Conceicao, 16, alisema Veron ndiye aliyemvutia zaidi wakati akifuatilia Kombe la Dunia la U-17 mwaka 2019. Wakati huo Veron alikuwa akiichezea Palmeiras, klabu ambayo Conceição pia anaitumikia katika akademi hiyo.

Uwezo wa nyota huyo, hasa chenga na mabao yake, ulimfanya kijana huyo kuwa miongoni mwa mashabiki wake.

Alisema wakati huo hakuwa na uhakika kama siku moja angepata nafasi ya kuwakilisha Brazil katika mashindano hayo, lakini sasa ndoto hiyo imetimia na anataka kutumia fursa hiyo kuonyesha uwezo wake.

“Nilikuwa nyumbani nikitazama Kombe la Dunia la mwaka 2019 kwa sababu Gabriel Veron alikuwa anacheza. Alikuwa Palmeiras na nilikuwa shabiki wake mkubwa. Nilivutiwa na ubora wake na mabao aliyofunga. Sasa ni mimi nimepata nafasi hii na ninaishi ndoto,” alisema Conceição.

Conceição ni miongoni mwa vijana wanaotazamwa katika kikosi cha Brazil kutokana na uwezo wake wa kucheza nafasi mbalimbali za ushambuliaji, akitumia kasi, chenga na ubunifu kuvuruga safu za ulinzi za wapinzani.

Akiwa amepitia akademi ya Palmeiras, kijana huyo amepitia hatua mbalimbali za soka la vijana na kupata nafasi ya kucheza katika vikosi vya umri tofauti.