Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Mainoo, Rashford, Bruno waiteka ‘shoo’ Old Trafford

SHOO Pict

Muktasari:

  • Hata hivyo, lisingekuwepo shangwe hilo kama kusingekuwa na viwango bora uwanjani na Kobbie Mainoo, Marcus Rashford na nahodha Bruno Fernandez waliteka shoo.

MANCHESTER, ENGLAND: JANA Jumapili, Uwanja wa Old Trafford ulikuwa ni full shangwe baada ya matokeo ya ushindi wa mvua ya mabao 5-2, dhidi ya Ipswich Town.

Hata hivyo, lisingekuwepo shangwe hilo kama kusingekuwa na viwango bora uwanjani na Kobbie Mainoo, Marcus Rashford na nahodha Bruno Fernandez waliteka shoo.

Maoinoo alianza kuiteka shoo baada ya kutambulishwa ikiwa ni mara ya kwanza anarejea kikosi cha kwanza baada ya kukosekana katika mechi dhidi ya Hull City na mtangazaji wa uwanja kumtambulisha mmoja wa wachezaji wa kikosi cha kwanza kwa maneno, “amezaliwa na kukulia Manchester.”

SHO 01

Hata hivyo, shangwe zaidi lilikuwa ndani ya uwanja kutokana na kiwango bora alichoonyesha akionyesha thamani yake baada ya kuongeza mkataba wa miaka mitano.

Licha ya Man United kutumia takribani Pauni 155 milioni kusajili viungo watatu msimu huu, lakini kiwango cha Mainoo kimedhihirisha nyota hao watakuwa na kazi ya kufanya kuiba namba na akiwa chini ya Kocha Michael Carrick, alikosekana katika mechi moja tu dhidi ya KLeeds msimu uliopita.

Nyota huyo aliyezaliwa Stockport anaonekana kuwa fiti msimu huu na kiwango chake kilisababisha mashabiki kumuimba muda wote wakilitaja jina lake.

SHO 02

RASHFORD AREJEA

Rashford alianza katika mechi hiyo ikiwa ni mara ya kwanza  baada ya siku 637.

Katika mechi hiyo, alichukua nafasi ya Patrick Dorgu ambaye hakuwa na kiwango, huku Benjamin Sesko hakuwa fiti baada ya kuumia mguu Mei 3, alishirikiana vyema na kuelewana na Matheus Cunha anayevaa jezi namba 10 aliyokuwa akiivaa Rashford kabla hajaondoka kwa mkopo na Cunha alimpongeza Rashford baada ya kumpa pasi iliyomwezesha kupata nafasi ya mapema. Kwa sasa Rashford anavaa jezi namba tisa iliyotambulishwa siku chache zilizopita na hata uwanjani na nje bado haijavaliwa kwa wingi.

Licha ya kipa wa Ipswich, Kjell Scherpen kumzuia Rashford mara mbili, lakini kiwango chake juzi kiliwafanya hadi mashabiki kusahau alivyowatibua na alisaidia kuzuia na kutengeneza mashambulizi.

Hata wakati akitolewa na Kocha Carrick pamoja na Mainoo, mashabiki hao walisimama na kupiga makofi wakipongeza juhudi zake alizoonyesha uwanjani.

SHO 03

FERNANDES BADO MWANANGWA

Pamoja na ujio wa nyota wapya, Fernandes bado ndiye kipenzi kikubwa cha mashabiki wa United na jina lake liliimbwa mara nyingi na kwa nguvu zaidi kuliko la mchezaji mwingine yeyote.

Kiungo huyo wa Ureno aliendeleakuthibitisha kwa nini anabeba hadhi hiyo baada ya kufunga hat-trick yake ya tatu akiwa United, na ya pili katika mchezo wa kwanza wa msimu uliofanyika Old Trafford.

Mabao yake, likiwamo la kusawazisha na lile la kufunga, yanaweza kuongeza presha kwa uongozi wa United kumlipa mshahara mkubwa zaidi kuliko Rashford.

Kwa sasa, hata hivyo, mchezaji anayeonekana kuwa bora zaidi United siye anayelipwa zaidi.