Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

MAGIC: Fundi mwingine anayetajirika baada ya kustaafu

ATM Pict

Muktasari:

  • Wiki kadhaa zilizopita tuliwahi kuweka stori ya Michale Jordan jinsi anavyoendelea kupata pesa na kutajirika licha ya kustaafu kucheza kikapu kwa muda mrefu.

CARLFONIA, MAREKANI: KATIKA mpira wa kikapu kwa sasa, wachezaji ambao wanaongoza kwa utajiri kijumla sio wale wanaocheza bali waliostaafu tena zamani.

Wiki kadhaa zilizopita tuliwahi kuweka stori ya Michale Jordan jinsi anavyoendelea kupata pesa na kutajirika licha ya kustaafu kucheza kikapu kwa muda mrefu.

Kwa mujibu wa tovuti mbalimbali, mchezaji wa kikapu wapili anayefuata kwa utajiri baada ya Jordan ni Magic Johnson ambaye pia amestaafu.

Tofauti na ilivyo kwa Jordan ambaye analipwa  na kampuni ya Nike kwa kutumia viatu vyenye jina lake, Magic yeye amekuwa tajiri kutokana na biashara zake alizoanzisha wakati anacheza kikapu na kuziendeleza zaidi baada ya kustaafu. Hapa tumekusogezea utajiri wake wote na jinsi anavyoendela kutajirika

AT 01

ANAPIGAJE PESA

Asilimia kubwa ya utajiri wake aliupata baada ya kustaafu mpira wa  kikapu. Magic alianzisha kampuni yake ya Magic Johnson Enterprises (MJE), ya uwekezaji. Ana utajiri unaokadiriwa kufikia Dola 1.5 bilioni.

Awali kupitia kampuni yake ya MJE alikuwa na hisa katika kampuni ya maduka ya kahawa (Starbucks) lakini aliziuza mwaka 2010.

Kupitia MJE, Magic pia amekuwa akishirikiana na kampuni ya SodexoMAGIC ambayo inamiliki  maduka ya rejareja, na nyumba za kupangishwa.

 MJE ndio chanzo kikuu cha mapato cha fundi huyu na kwa mwaka kupitia uwekezaji unaofanyika katika sekta mbalimbali humpatia takribani Dola 300 milioni.

Kupitia MJE, Magic anamiliki pia kampuni ya bima ya EquiTrust Life Insurance ambayo ni sehemu ya mapato yake.

Anamiliki hisa pia katika timu za mpira wa kikapu ambazo ni Los Angeles Dodgers, Los Angeles Sparks (WNBA), LAFC (MLS), pia ana hisa katika timu ya Rugby ya Washington Commanders (NFL) na timu ya soka la wanawake ya Washington Spirit (NWSL).

AT 04

NYUMBA

Anamiliki nyumba maeneo ya Beverly Hills, Tuscan na  Orange, California ambazo kwa pamoja zinakadiriwa kuwa na thamani ya Dola 25 milioni.

Aliwahi kumiliki nyumba pia maeneo ya Hawaii, lakini aliiuza na kununu mjengo uliopo  Beverly Hills.

Vilevile alikuwa akimiliki mjengo huko Bel-Air, alikoishi kuanzia mwaka 1981 hadi 1990 na akaiuza mwaka 2023 kwa Dola 11.5 milioni. Nyuma hii aliinunua kwa Dola 600,000.

AT 02

MSAADA KWA JAMII

Canyon-Johnson Urban Fund mfuko wa uwekezaji wa miji ulioundwa ili kuwekeza kwenye maendeleo ya miji na miradi ya real estate yenye athari ya kijamii. Mradi huu umewekeza mamilioni katika maendeleo ya jiji.

AT 03

NDEGE

Anamiliki ndege yake binafsi aina ya  Gulfstream III (G-III), yenye namba ya usajili ya N32MJ na imetengenzwa mwaka 1982. Ndege ambayo ndio amekuwa akiitumia katika safari zake mbalimbali ina thamani ya Dola 3 milioni.

AT 05

NDINGA

Rolls-Royce Phantom Drophead Coupe-Dola 500,000

Bentley Continental GTV V8 convertible-Dola 254,000.

Bentley Bentayga-Dola 250,000.

2023 Cadillac Escalade Sport Platinum-Dola 105,000.

Lincoln Mark LT Dove Edition-Dola 64,000.

Mercedes-Benz SL450-Dola 89,150

Lincoln Navigator-Dola 116,000

GMC Yukon-Dola 76,000

AT 07

MSAADA KWA JAMII

Magic Johnson amekuwa akisaidia sana jamii kupitia taasisi yake ya Magic Johnson Foundation (MJF) iliyozinduliwa mwaka 1991.

Taasisi hii imekuwa ikiandaa kliniki za  vipimo vya HIV/AIDS, kliniki za kupima magonjwa mbalimbali pamoja na kufadhili matibabu ya watu wasiojiweza.

Vilevile kupitia taasisi hii, Magic hutoa misaada ya elimu kwa watoto wa kimaskini na wale ambao wanaotoka katika mazingira magumu ndani ya Marekani na Afrika.

Ndani yake kuna mfuko wa Canyon-Johnson Urban Fund ambao huwa unatoa pesa kujenga miradi ya kijamii kama Hospitali na shula katika nchi zinazoendelea.

AT 06

MAISHA NA BATA

Yupo katika ndoa na Cookie Johnson tangu mwaka 1991 na wamebahatika kupata watoto wawili wakike ambao ni Earvin na Elisa Johnson, pia wana mtoto mwingine wakiume aitwaye Andre.

Magic sio mtu wa bata na muda mwingi ameuwekeza katika biashara zake na hiyo inadaiwa kuwa moja kati ya siri za kupata mafanikio aliyonayo sasa.