Mademu wa wanasoka wasiotegemea hela za waume zao
Muktasari:
- Hata hivyo, hiyo ni nusu tu ya ukweli halisi. Kuna wachumba wa wanasoka wapo vizuri kwelikweli kiuchumi. Pochi zao zimenona, cheki mkwanja walionao hapa chini:
LONDON, ENGLAND: IMEZOELEKA kwa imani kwamba wake na wachumba wa mastaa wa soka duniani wamekuwa wakiponda raha na kula bata wanavyotaka wakitumia pesa za wenza wao.
Hata hivyo, hiyo ni nusu tu ya ukweli halisi. Kuna wachumba wa wanasoka wapo vizuri kwelikweli kiuchumi. Pochi zao zimenona, cheki mkwanja walionao hapa chini:
1. Victoria Beckham - Dola 70 milioni
Mrembo Victoria ni mke wa gwiji wa Manchester United na staa wa zamani wa Real Madrid, David Beckham. Amevuna pesa zake kupitia muziki na mitindo ya mavazi.
2. Pilar Rubio Ramos - Dola 59 milioni
Mrembo Rubio ameolewa na gwiji wa Real Madrid, Sergio Ramos. Ni mtangazaji wa televisheni huko Hispania akisimia kipindi cha komedi na ni mwanamitindo pia.
3. Anna Lewandowska - Dola 45 milioni
Straika wa Barcelona, Robert Lewandowski amekuwa na ndoa yenye mafanikio na mrembo Anna Lewandowska. Anna amekuwa akipiga pesa kupitia masuala ya lishe na ana gym yake Barcelona.
4. Leigh-Anne Pinnock - Dola 25 milioni
Mrembo Leigh-Anne ni mpenzi wa staa wa zamani wa Ligi Kuu England, Mjamaica, Andre Gray.
Anne amevuna pesa zake kupitia biashara ya vipodozi, mitindo na muziki.
5. Antonela Roccuzzo - Dola 20 milioni
Supastaa Lionel Messi hahitaji utambulisho kwenye soka. Lakini, mkewe pia, mrembo Antonela naye ni maarudu sana, akipiga pesa nyingi kupitia ubalozi wa kampuni tofauti.
6. Coleen Rooney - Dola 19 milioni
Mrembo Coleen ni mke wa gwiji na supastaa wa England, Rooney. Mrembo huyo ni mhamasishaji na amekuwa akivuna pesa za kutosha kupitia dili mbalimbali za matangazo ya biashara.
7. Becky G - Dola 17 milioni
Mrembo Rebecca Gomez maarufu kama Becky G amekuwa kwenye uhusiano na mkali wa FC Dallas na kiungo wa zamani wa West Ham United, Sebastian Lletget. Anapiga pesa kupitia muziki.
8. Ana Ivanovic - Dola 17 milioni
Mrembo Ana Ivanovic ameolewa na gwiji wa Bayern Munich na Ujerumani, Bastian Schweinsteiger. Ivanovic ni mcheza tenisi ambaye amenasa dili nyingi za kumwingizia kipato.
9. Edurne Garcia - Dola 17 milioni
Mrembo Edurne amefunga ndoa na jipa wa zamani wa Man United, anayedakia Fiorentina kwa sasa, David de Gea. Mrembo huyo amepiga pesa kupitia muziki.
10. Perrie Edwards - Dola 15 milioni
Mrembo Perrie Edwards ameolewa na staa wa zamani wa Liverpool na Arsenal, Alex-Oxlade Chamberlain. Mrembo huyo anavuna pesa nyingi na kupata kipato chake kupitia muziki.