Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Maajabu ya Indiana Pacers fainali ya kibabe

NBA Pict

Muktasari:

  • Kwa mashabiki na wachambuzi wengi wa kikapu wanaitaja safari ya Indiana Pacers kusaka ubingwa hadi fainali za  ilikuwa ya kibabe na kusisimua zaidi. Hiyo ilikuwa ni safari ndefu kwa Pacers katika harakati iliyodumu hadi mchezo wa saba.

OKLAHOMA, MAREKANI: MWAKA 2025 umeshamalizika ukiacha kumbukumbu flani tamu na chungu kwa mashabiki wa Ligi ya Kikapu Marekani (NBA). Lakini, ni kumbukumbu gani ya michuano hiyo mwaka jana uliyoipenda na utabaki ukiikumbuka zaidi?

Kwa mashabiki na wachambuzi wengi wa kikapu wanaitaja safari ya Indiana Pacers kusaka ubingwa hadi fainali za  ilikuwa ya kibabe na kusisimua zaidi. Hiyo ilikuwa ni safari ndefu kwa Pacers katika harakati iliyodumu hadi mchezo wa saba.

Bila kuikosea heshima Milwaukee Bucks, Cleveland Cavaliers, New York Knicks au Oklahoma City Thunder wapinzani ambao Pacers waliwafunga au kukabiliana nao barabara katika kinyanganyiro hicho, lakini ubora zaidi ulikuwa katika namna walivyoweza kupanda kwa kushtukiza kutoka nafasi ya nne katika Ukanda wa Mashariki.

NB 01

Haikutarajiwa, ilisisimua, kuburudisha na yote hayo ndiyo Pacers waliyoambulia ikizingatiwa kwamba waliwashinda wapinzani wao wa jadi, Bucks, katika raundi ya kwanza kisha wakawafumua Cavaliers waliokuwa vinara wa Mashariki kwa michezo mitano katika nusu fainali.

Baada ya hapo walionyesha uimara na uwezo wa kucheza chini ya presha dhidi ya Knicks kwenye fainali za Mashariki, jambo lililoonekana ni kama kurejea kwa kishindo wakiwa nyuma kwa pointi 14, huku zikiwa zimesalia dakika tatu za mchezo wa kwanza kumalizika. Hata hivyo, walilazimisha muda wa nyongeza kwa mtupo wa ajabu wa mwisho wa Tyrese Haliburton, kisha wakashinda katika muda wa nyongeza.

NB 02

Kuna mashabiki pia wanaoizungumzia safari ya Pacers kuwa ilikuwa ni sawa na kushikwa na mkono wa ajabu. Ingawa biashara ya Luka Doncic kwenda Los Angeles Lakers na ubingwa wa Oklahoma City Thunder huenda yakawa matukio makubwa mwaka jana, kumbukumbu nyingine tamu inabaki kwa Pacers iliyoibuka washindi wa pili.

Katika safari yao hadi fainali za NBA, Pacers walicheza kila mechi kama fainali. Mchezo wa kwanza wa fainali ya Mashariki uliopigwa katika Uwanja wa Madison Square Garden ulikuwa moto. Wakiwa nyuma kwa pointi 17 katikati ya robo ya nne, Aaron Nesmith alitupia mipira sita ya pointi tatu katika dakika tano za mwisho.

Kwa wengine kilichowashangaza juu ya timu hiyo ilikuwa rekodi ya ushindi 16 na vipigo 18 siku kadhaa kabla hata fainali za Mashariki hazijaanza. Hata hivyo, miezi mitano baadaye walikuwa wakienda fainali dhidi ya moja ya timu bora zaidi katika historia ya NBA, Oklahoma, wakiilazimisha ngoma iende hadi mchezo wa saba.

NB 03

Pamoja na ubabe wa Oklahoma, simulizi na kumbukumbu nzuri inabakia jinsi walivyohenyeshwa na Pacers kuusaka ubingwa hadi kuupata kwani walilazimika kukipiga michezo yote saba.