Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Vipigo vitatu Lakers vyatibua mambo

NBA Pict

Muktasari:

  • Ni kutokana na vipigo hivyo na ushndi wa tofauti ya pointi nane katika mechi ya mwisho ndivyo vilivyomchefua kocha kijana wa kikosi hicho ambaye ameapa lolote linaweza kutokea ifikapo mwisho wa msimu huu.

LOS ANGELES, MAREKANI: VIPIGO vitatu mfululizo ilivyovipata Los Angeles Lakers dhidi ya Houston Rokects, Los Angeles Clippers na Phoenix Suns kabla ushindi dhidi ya Utah Jazz vimebakiza donge kwa kocha wa kikosi hicho, Jonathan Clay ‘JJ’ Redick ambaye anafikiria kuuza baadhi ya mastaa dirisha  lijalo.

Lakers ilichapwa na Rockets kwa pointi 119-96, Suns 132-108 na 103- 88 kutoka Clipers kabla ya kuilalia Utah 143-135 na kesho ikitarajiwa kuikaribisha Sacramento Kings katika mchezo wa Ligi ya Kikapu Marekani (NBA), imeanza kupotea taratibu katika mbio za kusaka ubingwa wa Kanda ya Magharibi kwenye msimu mrefu wa mashindano hayo.

Ni kutokana na vipigo hivyo na ushndi wa tofauti ya pointi nane katika mechi ya mwisho ndivyo vilivyomchefua kocha kijana wa kikosi hicho ambaye ameapa lolote linaweza kutokea ifikapo mwisho wa msimu huu.

“Tutauza, tutauza, tutauza... subirini,” alisema.

Kinachoelezwa ni kwamba JJ amechukizwa na namna mastaa wakubwa wa kikosi hicho wanavyocheza kana kwamba hawataki, akilinganisha uwezo wao na watoto wanaojifunza kikapu kwenye vituo vya kufundishia. 

NB 01

JJ ameonekana kuwarushia mpira wa lawama mastaa wakubwa wawili kikosini Luka Doncic na LeBron James aliyerejea hivi karibuni akitokea kwenye majeraha ya muda mrefu, ambapo ameelezea vipigo walivyopokea kwa wapinzani watatu kama mzaha uliotengenezwa na wazazi dhidi ya watoto wao.

Kocha huyo aliyeonekana mwenye hasira juzi kufuatia Lakers kufungwa na Rockets siku ya Krismasi, alidai hakukuwa na furaha ya sikukuu kwa sababu watu wachache waliamua iwe hivyo. Hicho kilikuwa kipigo cha sita kwa Lakers katika mechi 10 zilizopita.

“Hatujali vya kutosha kwa sasa. Na hilo ndilo jambo linalokasirisha. Hatujali vya kutosha kufanya mambo yanayohitajika. Hatujali vya kutosha kuwa bora uwanjani,” alisema JJ.

Kuporomoka kwa kiwango cha Lakers ni jambo la kushangaza ikilinganishwa na mwanzo mzuri wa msimu walioanza nao wakianza kwa rekodi ya ushindi wa 15-4 katika michezo 19 ya kwanza wakiongozwa na safu bora ya ushambuliaji chini ya Doncic.

NB 02

Hata hivyo, ingawa hawezi kulaumiwa peke yake, tangu LeBron aliporejea kutoka kwenye majeraha Lakers inaonekana kujikongoja kwani dhidi ya Rockets alifunga pointi 18 huku timu ikizidiwa kwa pointi 33 katika dakika 34 akiwa  uwanjani.

Hiyo ilikuwa rekodi yake mbaya zaidi ya ‘plus-minus’ tangu ajiunge na Lakers, na pia ilikuwa mechi ya tatu mbaya zaidi katika msimu wake mzima wa miaka 23 katika NBA.

Takwimu za Lakers zinaonyesha kwamba Doncic ameshuka kwa asilimia sita tangu LeBron aliporejea kikosini, na mfumo wao wa ushambuliaji uliokuwa huru unaonekana kusuasua na usio na nguvu.

Hali hiyo ilidhihirika dhidi ya Rockets, kwani wapinzani wao walijikuta wakiongoza kwa pointi 14 katika robo ya kwanza na hawakuuachia uongozi katika mechi ambayo haikuwa na ushindani wowote.

“Tunakuwa timu mbaya sana. Na tulikuwa timu mbaya sana. Na hilo lilianza mapema kabisa. Tuna wachezaji ambao hawataki kujiandaa. Na ni wazi kabisa ni kina nani hao...” alisema kocha huyo.

Lakers wanapokuwa wabaya, wanakuwa wabaya kupita kiasi, kwani vipigo vyote 10 walivyopata msimu huu vimekuwa kwa tofauti ya pointi 10 au zaidi.

NB 03
NB 03

Bila kutaja majina, Redick alidokeza kuwa kuna wachezaji katika timu hiyo ambao hawajiandai ipasavyo kukabiliana na wapinzani wao katika mechi.


DONCIC ATAKA MABADILIKO

Baada ya mechi, Doncic alikaririwa akisema hali itakuwa ngumu zaidi Lakers huku akitaka mabadiliko yafanyike.

“Sijui ni nini hasa kinapaswa kubadilika, lakini kwa hakika kuna kitu kinahitaji kubadilika,” alisema na kuongeza:

“Nadhani tumepigwa vibaya katika michezo mitatu iliyopita. Ni mbaya sana. Tunapaswa kutafuta suluhisho, hilo ndilo jambo tunalopaswa kufanya. Tunapaswa kulizungumzia. Kila mtu lazima azungumze. Najua JJ alisema hakutakuwa na raha wala amani kwa kila mtu. Kila mtu lazima aongeze juhudi kuanzia kwangu.”

Lakers itaikaribisha Sacramento Kings kesho Jumatatu katika mechi ambayo bila shaka itakuwa kipimo kingine kikubwa kwa JJ kubadili mfumo na uchezaji wa kikosi hicho.