Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Liverpool yatega kijanja kwa Isak

Muktasari:

  • Fowadi huyo wa kimataifa wa Sweden anatazamwa kama usajili muhimu wa Liverpool kwenye dirisha hili la majira ya kiangazi ikiwa ni mkakati wa kutengeneza washambuliaji kiwembe.

LIVERPOOL, ENGLAND: LIVERPOOL ipo tayari kuvutavuta muda kwenye mchakato wa kunasa saini ya mshambuliaji wa Newcastle United, Alexander Isak.

Fowadi huyo wa kimataifa wa Sweden anatazamwa kama usajili muhimu wa Liverpool kwenye dirisha hili la majira ya kiangazi ikiwa ni mkakati wa kutengeneza washambuliaji kiwembe.

Straika wa sasa, Darwin Nunez anahusishwa na mpango wa kutimkia Napoli ya Italia, hivyo atafanya kuwepo na nafasi ya kuziba huko Anfield.

Lakini, dili hilo linaonekana kuwa gumu baada ya Newcastle kuonekana kutokuwa na mpango wa kuuza mchezaji wao, huku ikibainisha bei yake kuwa ni Pauni 150 milioni.

Liverpool sasa inaonekana kuwa na mpango wa kutaka kukamilisha dili hilo kwenye dakika za mwisho kabisa. Ripoti zinafichua kwamba mabosi wa Liverpool wanafuatilia kwa karibu mchakato unavyokwenda ili kuona ifanye nini katika kukamilisha mpango wao.

Wanachoamini mabosi wa Liverpool ni kwamba itafika wakati Newcastle itahitaji pesa, hivyo itamweka staa wao huyo sokoni. Newcastle yenyewe ipo sokoni kufukuzia wachezaji James Trafford, Anthony Elanga na Joao Pedro - hivyo kuvuna mkwanja wa Pauni 100 milioni na ushee kwenye mauzo ya Isak utawasaidia kukamilisha dili zao hizo za wachezaji watatu.

Hata hivyo, Newcastle mpango wao wa kwanza ni kumbakiza Isak uwanjani St James’ Park na ndiyo iliwahi kuripotiwa kwamba wanataka kumfanya kuwa mchezaji anayelipwa mshahara mkubwa kwenye klabu hiyo ili kumfanya asishawishike kwenda Liverpool.