FIFA yaitosa rufaa ya Hossam Hassan na nduguye
Muktasari:
- Hossam alikuwa kocha mkuu wa timu ya taifa ya Misri, huku mdogo wake, Ibrahim Hassan, akiwa mkurugenzi wa timu hiyo kabla ya kuondoka kwao.
Kamati ya Rufaa ya Shirikisho la Soka la Kimataifa (FIFA) imetupilia mbali rufaa ya aliyekuwa kocha mkuu wa timu ya taifa ya Misri, Hossam Hassan, na aliyekuwa mkurugenzi wa timu hiyo, Ibrahim Hassan, dhidi ya adhabu ya kufungiwa mechi tatu kila mmoja.
Kamati ya Rufaa ya Shirikisho la Soka la Kimataifa (FIFA) imetupilia mbali rufaa ya aliyekuwa kocha mkuu wa timu ya taifa ya Misri, Hossam Hassan, pamoja na aliyekuwa mkurugenzi wa timu hiyo na ndugu yake, Ibrahim Hassan, kupinga adhabu ya kufungiwa mechi tatu kila mmoja.
Uamuzi huo unamaanisha kuwa adhabu zilizotolewa awali na Kamati ya Nidhamu ya FIFA zitaendelea kutekelezwa, huku uamuzi wa Kamati ya Rufaa ukiwa wa mwisho na wa lazima kwa wahusika.
Kwa mujibu wa uamuzi huo, adhabu hizo zitaanza kutekelezwa pale watakapopata nafasi nyingine ya kuinoa au kuisimamia timu ya taifa ya wakubwa ya chama chochote cha soka.
Hali hiyo inawafanya makocha hao wawili kusubiri kupata timu nyingine ya taifa watakayofanya nayo kazi ili kuanza kutumikia adhabu zao, baada ya Shirikisho la Soka la Misri kuachana nao.
Hossam alikuwa kocha mkuu wa timu ya taifa ya Misri, huku mdogo wake, Ibrahim Hassan, akiwa mkurugenzi wa timu hiyo kabla ya kuondoka kwao.
Adhabu hizo zilitolewa kufuatia malalamiko yao dhidi ya maamuzi ya waamuzi baada ya Misri kutolewa na Argentina katika hatua ya 16 bora ya Kombe la Dunia 2026, mchezo uliomalizika kwa Argentina kushinda mabao 3-2.
Baada ya mchezo huo, Hossam Hassan na Ibrahim Hassan walikosoa maamuzi ya waamuzi, wakidai kuwa yalichangia kuiondoa Misri katika mashindano hayo.