Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

MC Alger yaachana na kocha Ben Yahia ikiisubiri Yanga

Aliyekuwa kocha wa MC Alger, Khaled Ben Yahia.

Muktasari:

  • Ben Yahia alifikia uamuzi huo baada ya MC Alger kupoteza mchezo wake wa nyumbani kwa bao 1-0 dhidi ya Olympique Akbou, Novemba 19, 2026

Wakati Yanga ikijiandaa kuikaribisha MC Alger katika mchezo wa hatua ya makundi ya Ligi ya Mabingwa Afrika, wapinzani wao hao wameachana na kocha wao, Khaled Ben Yahia.

Ben Yahia amejiuzulu kufuatia shinikizo lililotokana na mwenendo usioridhisha wa timu hiyo katika Ligi Kuu ya Algeria msimu huu.

Ben Yahia alifikia uamuzi huo baada ya MC Alger kupoteza mchezo wake wa nyumbani kwa bao 1-0 dhidi ya Olympique Akbou, Novemba 19, 2026.

Kocha huyo raia wa Tunisia aliwasilisha uamuzi wake kwa uongozi wa klabu Novemba 20, siku moja baada ya kipigo hicho.

Katika michezo nane ya Ligi Kuu ya Algeria iliyokuwa imecheza hadi Novemba 19, MC Alger ilikuwa imekusanya pointi 16 na kushika nafasi ya tano kwenye msimamo wa ligi,ikifunga mabao tisa na kuruhusu mabao matatu.

Leo itakuwa ugenini kuikabili JS Kabylie katika mchezo wa Ligi Kuu ya Algeria, ikiwa chini ya kocha msaidizi wa timu hiyo, Karim Delhoum.

Mchezo huo utapigwa katika Uwanja wa Hocine Ait Ahmed, Tizi Ouzou, kuanzia saa 3:00 usiku kwa saa za Tanzania.

Kwa upande mwingine Yanga, ipo katika nafasi ya pili kwenye msimamo wa Ligi Kuu Tanzania Bara, baada ya kucheza mechi 11, imeshinda tisa, sare moja na kupoteza mechi moja. Imefunga mabao 25 na kuruhusu matano.

MC Alger itasafiri Tanzania kwa ajili ya kukutana na Yanga Jumamosi, Novemba 28, katika mchezo wa hatua ya makundi ya Ligi ya Mabingwa Afrika utakaochezwa kwenye Uwanja wa New Amaan Complex, Zanzibar.